Mkuu pole sana. Kwanza mara nyingi hali hii humtokea mtu ambaye hachoki,yani unaenda kulala tu. Ktk hali iyo unakuta unawaza mambo mengi na ukiwa gizani,hapa waweza kuruhusu akili ifanye unavofikiria ndo mana inakuwa ivo ivo. Kwa iyo jitahidi kuwa bize mchana ili ukienda kulala upate usingize wa kweli au fanya mazoezi ya mwili. Mfano,japo hujasema ila hujiulizi kwa nini hutokea mida ya sa8 kasoro mpaka sa9 pekee?na unapolala unashtuka umekabwa na ukiamka hamna kitu! Ukilala tena ivo ivo ukshtuka hamna kitu! Kwa nini ukilala kuanzia sa3-7 haijitokezi na sa10 mpaka asubuhi hamna kitu. Hapa utaambiwa na waabudu mizimu eti kwa sababu majini yanapenda usiku wa manane,wapi! Pia kwa kuwa una imani uliyoitaja basi ni vema pia ukajaribu kuwa na maji yaliyobarikiwa na kiongoz wa kiroho,yan maji ya baraka pamoja na biblia chumbani mwako. Pia kama haupati usingizi vizuri na kuhisi umebanwa,jitahidi kufungua dirisha au pazia nzito ili upate hewa safi,na ikiwezekana weka maji kwenye beseni mbili au zaidi weka karibu au chini ya kitanda,utakuwa umeongeza oksijeni na utalala vizuri bila kuisi kubanwa wala kuona jinamizi. Najua unasumbuka kwani hali hiyo ikitokea yani unahisi hata kuongea ,kunyanyua hata kichwa haiwezekani kabisa na wakati mwingne ukiamka hata kichwa kinauma. Usiende kwa waganga watakutupia majini na pepo wachafu,usikubali kujiweka ktk mikono ya shetani. Ushauri wangu waweza kukusaidia kwa sababu umewasaidia wengi.
Huyu mheshimiwa ndio kamaliza shida yako.
Hali uliyonayo umeielezea kama vile upo kichwani kwangu kwa sababu matatizo kama hayo nimepata sehemu kubwa ya maishani mwangu. Tofauti ni kwamba mimi naelewa jinsi ya kujiepusha.
Kwa sasa hivi ninafahamu hata jinsi mtu unavyopata jinamizi. Sio uchawi wala majini. Jinamizi (Nightmare) ni ndoto mbaya tu.
Shule yake inahusisha mambo ya mfumo wa fahamu (nervous system) na inavyocontrol muscle movement pamoja na consciouness.
Kifupi ni kwamba unatakiwa ulale bila kuwa na HOFU YOYOTE au mawazo/msongo wa mawazo. Jitahidi kujiridhisha rohoni kuwa hamna kibaya cha kukutokea, lala ukiwa na amani rohoni. Basi hapo hutapata jinamizi.
Ukiongea na wazee watakwambia ni wachawi wanakukandamiza, na kwamba ulale na mkaa kwenye pillow, au uweke bible, au kemea... Hayo yote yanafanikiwa baada ya wewe kuamini kuwa yanafanya kazi na hivyo kukuondolea hofu na kukupa amani, utalala bila jinamizi. Lakini ukweli ni kuwa hamna cha mchawi wala jini. Ni hofu yako tu ina play tricks in your mind. Ondoa hofu. Utalala.
Rafiki yangu mwingine alihamia mitaa fulani pale sinza, akawa ameambiwa kuna jirani mchawi. Basi mapaka yalikuwa yakipiga kelele usiku, akawa anaingiwa na hofu akifikiri "wenyewe" wamekuja. Akawa anapata majinamizi kila siku akiamini ni wachawi wanakandamiza. Mpaka nilipomuelewesha suala la kuondoa hofu, akaanza kulala vizuri na kukubali kuwa kelele za paka hazina uhusiano na wachawi.
Hiyo hapo juu iendane na kufanya mazoezi ili uchoke. Muda wote ukiwa umechoka sana, hupati jinamizi.
Kama unataka kujua zaidi, ni PM.