last week nili drive kutoka dodoma kuja dar cha ajabu askari wa usalama barabarani wenye tochi walikuwa wengi mno hadi unashindwa ku enjoy drivin. wakati nakaribia mikese kuna kibao cha 50km/h so nikapunguza spidi cha ajabu jamaa akapiga tochi akanikamata eti akasema nilkua naendesha 52km/h so natakiwa nilipe faini tshs 30,000 kwa kweli nilikataa hadi likawa zogo kubwa. pale wakikuwepo pia askari wengine na land rover yao ndo wamefanya ofisi wanalipisha fine wakanishauri nilipe ili nisipelekwe mahakamani but sikukubali baadae wakaniacha pale kila mmoja akaenda na shughuli zake na mimi nikachapa mwendo. swali langu kwenu ni je vile vibao vya 80,50,na 30 km/h je vinamaanisha below hiyo namba au within that number ?