Msaada wana jf - tax exemption kwa mfanyakazi serikalini

Msaada wana jf - tax exemption kwa mfanyakazi serikalini

Muhubiri

Senior Member
Joined
Mar 11, 2012
Posts
140
Reaction score
120
Naomba msaada tafadhali, nimeagiza gari na limefika bandarini jana, kodi imekua kubwa, ni Toyota Premio ya mwaka 2003, cc 1500, kodi ni mil 8, Je, utaratibu wa msamaha wa kodi kwa mfanyakazi wa serikali ukoje? na unapitia hatua zipi?
Natanguliza shukurani.
 
Mbona nilisikia hiyo misamaha ya kodi kwa wafanyakazi wa serikali iliishafutwa? Na hiyo kodi ya milioni 8 kwa gari la mwaka 2003 kama ni kubwa sana? Au tayari limezidi miaka 10 na wamekuchaji uchakavu pia?

Tiba
 
mkuu hukujua au ni uzembe wa clearing agent wako? yaani gari hadi linaingia bandarini bado hujashughulikia exemption tu!

hata ukianza kushughulikia j3 hadi upate, hizo storage charges zitakuwa za kufa mtu. Binafsi nakushauri ulipie tu uchukue gari lako fasta kabla storage haijaongezeka

halafu ujue kodi imekuwa kubwa kwa sababu umepigwa uchakavu, gari lako ni 10 years old. Na uchakavu hauna exemption
 
Ilikua na uchakavu, ila ni kuwa thamani ya kununulia na kodi hazitofautiani sasa? kweli nchii hii haifai
 
Huo ni uzembe wa juu wa clearing agents..

Ndio maana mimi nasemaga bora ufate kampuni za kueleweka zikufanyie clearance kama DHL, SDV au K+N, hata kama gharama zao ni kubwa lakini uzembe kama huu storage wanalipia wenyewe..

Vitu vyote muhimu vinatakiwa vifanyike wakati goods ipo kwenye maji meli inapofika dar ni kufanya final assesment, kulipia kodi na kutoa mzigo fasta..

Usipojua jinsi ya ku monitor clearing agents utalia kila siku..
 
Bwana muhubiri kwanza pole sana,ushuru pale Bandarini kwa sasa ni hatari,ukienda showroom za nchi zisizo na Bandarini Kama Rwanda,Burundi,Uganda nk magari unaweza kununua kwa bei ndogo kuliko sisi wenye bandari.Siku hizi watu wanatoka hapa TZ (kwenye bandari)wanakwenda Uganda (kusipo na bandari)kununua nguo za biashara !!!!nilileta mada siku za nyuma kidogo nikilaumu ushuru mkubwa unaotozwa pale Bandarini lakini baadhi ya wachangiaji walinibeza sana.
Bwana muhubiri Kama TZ ikiwafanyia wazawa Kama wanigeria walivyowafanyia wazawa wake tusingesumbuka na ajira,Nigeria kuna punguzo kubwa sana la kodi kwa wazawa ndio maana ukienda miji ya kibiashara duniani utakutana nao wengi sana,wananunua bidhaa na kutuma Nigeria Leo hii nchi nyingi za Afrika magharibi shopping Yao kubwa ni Lagos.
Suala lako la punguzo la kodi litachukua mda mrefu sana Mpaka kukamilika hivyo Kama Mito alivyokushauri storage itakuwa kubwa sana,pili gari lililo na sifa za punguzo linatakiwa liwe chini ya miaka 10 at least 2004 model...suala la exemption(punguzo la kodi)bado lipo lakini Lina process ndefu na punguzo ni dogo sana,Mwaka juzi niliingiza Rav 4 kwa punguzo nililipa 6ml....
 
Kweli kabisa Lucky Sabasaba, Umeongea nadhani watu walikubeza kwa sababu hawakujua hali halisi, ila ukweli ni kuwa kuna umuhimu wa kubuni vyanzo vingine vya mapato nasio magari tu, hilo likitanguliwa na mfumo wa ukokotoaji wa kodi.
Nashukuru kwa hekima yako
 
Naomba msaada tafadhali, nimeagiza gari na limefika bandarini jana, kodi imekua kubwa, ni Toyota Premio ya mwaka 2003, cc 1500, kodi ni mil 8, Je, utaratibu wa msamaha wa kodi kwa mfanyakazi wa serikali ukoje? na unapitia hatua zipi?
Natanguliza shukurani.

Mbona hiyo bei ni kubwa ndugu. Kwani nimeingia kwenye Claculator yao iliyopo online hivi sasa KODI inatakiwa iwe ni Tshs 4,844,405 tu kwa gari kama hiyo. Ama unasema ni pamoja na bei ya kununulia? May be hiyo calculator mpya hawajaiweka bado wanaishikilia wao wenyewe lakini nafikiri uwe makini isije ikawa ni hao ma-agent ( Disclaimer " I hate them the most") wanakuchezea kukutoa upepo maana jamaa awakawii kukwambia toa 2M tukawaone TRA wakupunguzie na wao wanaiweka kibindoni. MJINI SHULE NDUGU yangu!!
[TABLE="width: 140"]
[TR]
[TD]
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
.
[TABLE="width: 111"]
[TR]
[TD]
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Kweli kabisa Lucky Sabasaba, Umeongea nadhani watu walikubeza kwa sababu hawakujua hali halisi, ila ukweli ni kuwa kuna umuhimu wa kubuni vyanzo vingine vya mapato nasio magari tu, hilo likitanguliwa na mfumo wa ukokotoaji wa kodi.
Nashukuru kwa hekima yako

Pia ushuru wetu ni wa makisiokisio tu,Leo ukituma hiki kodi ni hii kesho ukituma kile kile kodi ni tofauti kabisa !!!nilishangaa kuna siku niliagiza gari ikaja hesabu ya Tra Kama 4.5ml nilichukua ile document P PAD (Kama sijakosea)nikaenda pale Tra ghorofa ya kwanza kulikuwa na mzee mmoja alikuwa anasikiliza sana na ndiye anausika na mambo ya ushuru wa magari,baada ya kuongea naye (bila ata kumpatia CHAI) alinipunguzia 1.2ml,nilishangaa sana !!!! Yaaani ni maelewano !!!kuingiza Toyota Ist Tanzania ni ya Mwaka 2004 ni 4.5ml,Kuiingiza S Afrika ni tsh 3.1ml na gari hilohilo kuliingiza Nigeria ni Tsh 2.8 ml
 
Mbona hiyo bei ni kubwa ndugu. Kwani nimeingia kwenye Claculator yao iliyopo online hivi sasa KODI inatakiwa iwe ni Tshs 4,844,405 tu kwa gari kama hiyo. Ama unasema ni pamoja na bei ya kununulia? May be hiyo calculator mpya hawajaiweka bado wanaishikilia wao wenyewe lakini nafikiri uwe makini isije ikawa ni hao ma-agent ( Disclaimer " I hate them the most") wanakuchezea kukutoa upepo maana jamaa awakawii kukwambia toa 2M tukawaone TRA wakupunguzie na wao wanaiweka kibindoni. MJINI SHULE NDUGU yangu!!
[TABLE="width: 140"]
[TR]
[TD][/TD]
[/TR]
[/TABLE]
.
[TABLE="width: 111"]
[TR]
[TD][/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Bwana Nyati una point pale lakini gari hili dumping fee pekee ni almost 2ml(ilipandishwa toka 1/7)mbali na Vat,Import duty,na kodi nyingine...pia bado cost za Bandarini wanakuchelewesha makusudi ili storage ipande utasikia Leo system ipo down tusubiri kesho,oooh leo mtoa release hayupo!!!!kuna vituko pale
 
Nayo nimeiweka kwenye mahesabu tayari mdau akomae kuna kitu hapo.

ANGALI HII hapa chini Total Taxes in USG ni 3,028 ukitumia Ex rate ya 1,600/= ndo unapata hiyo bei ukitumia chini ya hapo unapata pungufu kidogo.

[TABLE="width: 631"]
[TR]
[TD="colspan: 7"]Motor vehicle with more than 1000cc but not exceeding 2000cc (Aged more than 10 Years)[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 3"]Example of vehicles: Toyota Mark II Model GX110, Toyota Corolla, Subaru forester, RAV4,Pajero Junior (io)[/TD]
[TD="colspan: 4"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 3"]GUIDELINE SUBJECT TO VERIFICATION[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 2"]Current Retail Selling Price[/TD]
[TD] 31,943[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 2"]Depreciation[/TD]
[TD]80%[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 2"]Freight[/TD]
[TD] 3,000[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 2"]Customs value[/TD]
[TD] 3,300[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 2"]FOB Value[/TD]
[TD] 300[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 2"]Import Duty 25%[/TD]
[TD] 825[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 2"]Excise Base for vehicle aged more than 10 years[/TD]
[TD] 1,031[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Excise Base[/TD]
[TD][/TD]
[TD] 4,125[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 2"]Excise Duty 5%[/TD]
[TD] 206[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 2"]VAT Base[/TD]
[TD] 5,363[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 2"]VAT 18%[/TD]
[TD] 965[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 2"]Total Taxes[/TD]
[TD] 3,028[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 2"]Total Taxes in TSHs[/TD]
[TD] 4,844,405[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Kwa mil 8 ndugu yangu wanakuibia mchana kweupee!! Hebu nenda ofisi za TRA kuomba maelezo ya ziada.
 
Bwana Nyati tatizo ni moja watu wengi wanachanganya hapa,moja ni kwamba wengi wanatazama CIF waliyotumia mfano $3000 kisha wanaotumia hiyo kwa calculation zao siyo hivyo hawa jamaa wa Tra wana Uplift CIF ndio maana kodi inakuwa kubwa(hapo bwana Nyati hatujui CIF TRA waliyotumia),bwana Nyati niliagiza Toyota IST ya 2004(haina dumping fee)ushuru ulikuwa almost 4ml,sasa hilo ni kubwa kwa IST na lina dumping fee..aende TRA lakini hiyo 4.8ml ni ndogo sana kwa system ya sasa ya TRA
 
Milioni 8 kwa ushuru na takataka zote za kuitoa kwa Toyota Premio ni kubwa sana. Lazima kuna kitu, nenda TRA ofisi upate maelezo ya ziada, haiwezekani hiyo gari ina estimated new price ndogo sana hivyo haiwezi kufika huko.
 
Back
Top Bottom