Msaada wanajamvi: Nakohoa damu tena nyingi

Sir Lugoje

Senior Member
Joined
Jan 9, 2014
Posts
169
Reaction score
54
Nilianza kukohoa nikiwa depo mwaka jana, nikapigwa xray lakini baado madaktari wa KCMC wakasema wameshindwa kujua ni nini.

Mwaka huu tena imetokea..huwa nikianza kukohoa kawaida mara damu inaanza kutoka hadi puani,sio na makohozi ni damu tu.

Nikaambiwa ni AC ya ofisini au feni ya gheto. Baadae nikaviepuka,nikajisahau siku moja nikaendesha pikipiki bila koti,nikakohoa damu mfululizo mpaka nikaenda regency hospital nikapigwa xray nikaambiwa kuna uhafifu kwenye pafu la kulia lakini hawajui ni tatizo gani,sio TB wala kansa.

Nikapewa strong antibiotic KOACT ndo nmeitumia wiki hii. Naendelea vizuri.

NAOMBENI MNISAIDIE KUJUA NI TATZO GANI. JE NI BARID YA KUKIMBIA AU KUENDESHA PIKIPIKI AU NI NINI?
 
Ni bora ukafanye vipimo tena mkuu sehemu nyingine majibu huwa yanatofautiana.Mungu akuponye
 

Kuna ugonjwa unaitwa Ugonjwa Dieulafoy huu pia unaweza kusababisha mtu kukohoa damu.
Au infection kwenye blood vessels za ndani ya MAPAFU.
Km una nafasi kidogo nenda india ukaganye FULL BODY CHECKED kwa chini ya dola $600 tu!

Ukitoka hapo unapewa Full report ya matatizo yako. Guarantee! Well almost Guaranteed!

Mungu akufanyie wepesi Mkuu.
Amin
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…