Okhondima
JF-Expert Member
- Jul 10, 2013
- 1,249
- 1,102
Salam ndugu,
Naomba kwa anayejua anijuze ni namna gani nitaweza kuwatibu kuku wangu wa kienyeji kutokana na ugonjwa unaowasumbua.Ugonjwa huo unawatokea kuku ghafla na moja a dalili zake ni kuku kugandiwa na kinyesi katika njia yake ya kujisaidia ambayo hali hiyo hupelekea kuku kudhoofu na matokeo yake sasa,utumbo humtoka nje kuku huyo kwa kupitia njia hiyo hiyo ya kutolea kinyesi.
Hali hiyo imenisumbua kwa muda sana,hata kupelekea kubadilisha banda,kuyasafisha mabanda na vyombo wanavyotumia kulia kuku ili kupunguza ama kuondosha kabisa tatizo hilo,lakini bado hali imeendelea kuwa mbaya zaidi.
Tatizo ni kuwa kuku wa jirani yangu hawapatwi na magonjwa hayo,ila nilipojaribu kuuliza niliambiwa kuwa hiyo inatokana na madhara wanayoyapata kutoka kwa kuku wa kisasa ambao nafuga.Zile dawa nazowapa kuku wa kisasa ndio zinawaathili hawa kuku wa kienyeji.
Sina ufahamu juu ya hilo ila kama kuna mtu anajua tiba ama chanjo ya tatizo anaweza kunisaidia.
Naomba kuwasilisha.
"Nlikuwepo":bolt: