Msaada wanajamvi

Okhondima

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2013
Posts
1,249
Reaction score
1,102
Salam ndugu,

Naomba kwa anayejua anijuze ni namna gani nitaweza kuwatibu kuku wangu wa kienyeji kutokana na ugonjwa unaowasumbua.Ugonjwa huo unawatokea kuku ghafla na moja a dalili zake ni kuku kugandiwa na kinyesi katika njia yake ya kujisaidia ambayo hali hiyo hupelekea kuku kudhoofu na matokeo yake sasa,utumbo humtoka nje kuku huyo kwa kupitia njia hiyo hiyo ya kutolea kinyesi.

Hali hiyo imenisumbua kwa muda sana,hata kupelekea kubadilisha banda,kuyasafisha mabanda na vyombo wanavyotumia kulia kuku ili kupunguza ama kuondosha kabisa tatizo hilo,lakini bado hali imeendelea kuwa mbaya zaidi.

Tatizo ni kuwa kuku wa jirani yangu hawapatwi na magonjwa hayo,ila nilipojaribu kuuliza niliambiwa kuwa hiyo inatokana na madhara wanayoyapata kutoka kwa kuku wa kisasa ambao nafuga.Zile dawa nazowapa kuku wa kisasa ndio zinawaathili hawa kuku wa kienyeji.

Sina ufahamu juu ya hilo ila kama kuna mtu anajua tiba ama chanjo ya tatizo anaweza kunisaidia.

Naomba kuwasilisha.

"Nlikuwepo":bolt:
 
Nadhani hiyo ni coccidiosis, ukiwapata wa kisasa wanakufa wengi. Kinga na tiba ni ancoban au amprolium wiki ya tatu vifaranga. Wakiumwa pia ni full dose. Usafi wa banda, maji na chakula. Kama unafuga wa kisasa ukitibia vifaranga uwatibu na hawa pia, ni kweli unaambukiza na kwa vile wakisasa hawana kinga kubwa wanaupata hivyo hawa wanautoa huko.
 
kuna uzi mmja hapa jamaa alijita dokta wa mifugo .alisema aulizwe swali lolote khsu ugugaji na tiba zake jaribu ku search
 
dah! Kumbe nawe ni mfugaji!....hongera zako mkuu
Nafuga mkuu,ila matatizo nayapata mengi nan ndio maana nikaamua kuingia humu kwa mara ya kwanza kabisa kuomba msaada.

"Nlikuwepo":bolt:
 
kuna uzi mmja hapa jamaa alijita dokta wa mifugo .alisema aulizwe swali lolote khsu ugugaji na tiba zake jaribu ku search
Nashukuru mkuu,nitajitahidi kumtafuta muhusika.

"Nlikuwepo":bolt:
 
Kuna mtu aliniambia nijaribu kulisafisha banda la kuku wa kisasa then niliache likiwa halina kitu kwa muda wa miezi mitatu,baada ya hapo ndio niendelee na ufugaji wa kuku wa kienyeji.
Hivi unafikiri hii inaweza kusaidia kama nikijaribu kufanya hivyo?

"Nlikuwepo":bolt:
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…