Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Jamani naombeni maelezo kuhusu mahakama ya kadhi
Ni hilo tuu
KATIBA INAYOPENDEKEZWA HAIJATAJA KUHUSU HIYO ISHU KWASABU NCHI HII HAINA DINI, HIVYO MAMMBO YA DINI YATASHUGHULIKIWA NA TAASISI ZA KIDINI PEKEE LAKINI KILA MTU ANA UHURU NA IMANI YA DINI YAKE, SOMA KATIBA INAYOPENDEKEZWA SEHEMU YA UHURU WA IMANI YA DINI KATIKA IBARA YA 41.
Sehemu hiyo inasomeka hivi:-
41.-(1) Kila mtu ana uhuru wa mawazo, dhamiri, imani na uchaguzi
katika mambo ya imani ya dini na anao uhuru pia wa kubadilisha dini, imani yake au kutokuwa na imani na dini.
(2) Kazi ya kutangaza dini, kufanya ibada na kueneza dini itakuwa ni
huru na jambo la hiari kwa mtu binafsi ilimradi hakiuki sheria za nchi.
(3) Shughuli ya uendeshaji wa jumuiya za dini itakuwa nje ya shughuli
za mamlaka ya Serikali.
(4) Hifadhi ya haki zilizotajwa katika Ibara hii itakuwa chini ya utaratibu
utakaowekwa na sheria ambazo ni muhimu katika jamii ya kidemokrasia kwa jamii ya kidemokrasia kwa ajili ya usalama, amani, maadili na umoja wa jamii na wa kitaifa na vitasimamiwa kwa utaratibu utakaoainishwa kwenye sheria za nchi.
(5) Ni marufuku kwa mtu, kikundi au taasisi ya dini kutumia uhuru wa
kutangaza dini kwa namna ambayo italeta uvunjifu wa amani, kujenga chuki au kuchochea vurugu na ghasia kwa madai ya kutetea imani au dini hiyo.
(6) Dini na imani ya dini haitatumika kwa namna yoyote itakayowagawa
wananchi, kuleta uhasama au uvunjifu wa amani miongoni mwa wananchi.
(7) Neno dini kama lilivyotumika katika Ibara hii litatafsiriwa kwamba
maana yake ni pamoja na madhehebu ya dini, na maneno mengine yanayofanana au kuambatana na neno hilo nayo yatatafsiriwa kwa maana hiyo.
hivi vifungu ni geresha tupu.katiba ya sasa haitambui dini lakini watawala huku wakijua hilo wanaleta mjadala wa mahakama ya kadhi bungeni halafu unatuletea vifungu vya uuongo mweupe