Msaada wanaoenda China

Adharusi

JF-Expert Member
Joined
Jan 22, 2012
Posts
14,422
Reaction score
7,350
Naomba kuonyeshwa ramani, mie nafanya biashara ya duka la vipodozi Tanzania na Msumbij, nimeamua kufungua duka la vifaa vya simu kwa jumla Msumbiji. Mfano kava, chaji za simu na laptop kwa ufupi vifaa mbalimbali vya simu, nilitaka wenye uzoefu wa kwenda China au Dubai niwasiliane nae aniambie jinsi ya kufanya yaani taratibu, passport ninayo na kule China maduka yako vipi, nitashukuru sana mwenye uelewa anaweza kumwaga hapa au aniPM ili tuwasiliane.
 
kweli wakuu ambao wanauelewa juu ya hl watuelezee coz 2po wengi tunaotaka kujua juu ya hili
 
Unataka kujua taratibu za kwenda..visa wawezapata toka kwenye shirika la ndege unalotumia mfano kwenda dubai ukikata emirates wana uwezo wa kukuandalia visa ndani ya siku 7 ikawa imekwishatoka maana emirates ni shirika la ndege la dubai...habari zaidi nenda kwa maagent wanaokatisha ticket(airline tickets)watakupa maelezo na bei kamili....unapokwenda dubai ujue ni hoteli gani cheap ya kufikia zipo za tsh 80,000/ na chini ya hapo..tatu jua sehemu cheap ya kuchukulia mzigo maana si dubai yote vitu ni cheap kuna maduka kwa ajiri ya wafanyabiz...kuna maduka ya watalii..kuna maduka ya wakazi na maduka ya waarabu hivyo lazima ujue maduka ya wafanyabiz wa kiafrika yalipo....dubai ni mji wa kibiashara kuwa makini sana kwa vijana wanaosema tukusindikize kukuonyesha vitu madukani mwuza duka akikuona na mtu vitu vitapanda bei kidogo yule aliyekupeleka atarudi baadaye kuchukua chake (hii ni muhimu sana)...pia jua season mfano sasa hivi maduka mengi ya electronics ya dubai yanafanya clearance hasa flat screen zinauzwa bei rahisi ili kuweka mzigo mpya sasa kwa wale wafanyabiz za electronics huu ndio wakati wao...so watakiwa kujua season...pia watakiwa kujua cargo gani ni cheap kwa kukutumia mzigo wako ulionunua...kama wataka kuja dubai waweza kunipm nikakuandalia kila kitu,ila inategemea ni lini umepanga kuja....dubai ni mji mdogo sana kama umepata maelezo mazuri hautasumbuka...karibu sana...sina uzoefu sana na china pia nawezakukutafutia contacts za watu wanaouza hivyo vitu utakavyo ukiongea nao wawezapata bei ya vitu kabda hujaja pia kama unachukua mzigo mkubwa wanawezakukuandalia visa huku ikawa rahisi zaidi...kumbuka unawezaandaliwa visa ata na hoteli utayofikia huku bei ikawa chini sana kuliko kuiandaa huko...visa ukikatia huku inakuwa $120 tu bila deposit yoyote
 
yeye anaulizia china nyie mnaleta habari za dubai. vipi bana?. mia
 
yeye anaulizia china nyie mnaleta habari za dubai. vipi bana?. mia

Figganigga soma maelezo yake kwanza kaka..hacha kuact as if you are amoung 60%...kaulizia china au dubai..mpe maelezo ya china basi
 
AHSANTE LUCKY SABASABA nitakutafuta,nipo msumbiji sasa,ila naendelea kusubili taarifa zaid,katikati ya mwezi nakuja TZ
 

winston
lucky xabaxaba naomba unijuze tafadhal nahitaj kujuwa Dubai zaid nataka kuja kuchukuwa mzigo huko wa jwerly , perfumes , watches , vipodozi whatsapp namba yng n +255719821774
 
Last edited by a moderator:
Nilikuwa sijui; kumbe mashirika ya ndege yanatafutia watu visa??
 

Mkuu mie nipo China, nadhani tunaweza kufanya business. Hebu njoo pm, tuongee fresh.
 
Mkuu mie nipo China, nadhani tunaweza kufanya business. Hebu njoo pm, tuongee fresh.

Weka mambo hadharani tujue labda watu wengine wanaweza kuwa interested
Mbona lucky kaweka mambo hadharani we unamvuta uchochoroni? Adhurus angalia mjini hapa.......
 

Kiongozi naomba nikutafute nadhani kuna mengi unaweza nisaidia....
 
Weka mambo hadharani tujue labda watu wengine wanaweza kuwa interested
Mbona lucky kaweka mambo hadharani we unamvuta uchochoroni? Adhurus angalia mjini hapa.......

Mkuu sio kila mtu mwizi, jaribu kuwapa watu benefit of doubt unless hutoweza kupanua network yako milele. Mie nataka kuongea naye proposal nyingine kama mbadala kama ataona inafaa. Ipo nje ya mada yake.
 
Mkuu sio kila mtu mwizi, jaribu kuwapa watu benefit of doubt unless hutoweza kupanua network yako milele. Mie nataka kuongea naye proposal nyingine kama mbadala kama ataona inafaa. Ipo nje ya mada yake.

Hakuna shida kiongozi, nilitaka tu uweke madini hadharan maana tupo wengi tuna vihela vyetu vidogo vya madafu hatujui tufanyie nn labda tunaweza pata mawazo mapya... Poa lkn sio issue.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…