Msaada: Wanauchumi nitawezaje kusave mshahara wa laki moja na ishirini, ili nami niwe na mafanikio?

Msaada: Wanauchumi nitawezaje kusave mshahara wa laki moja na ishirini, ili nami niwe na mafanikio?

Sigara Kali

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2017
Posts
3,623
Reaction score
8,442
Hili suala nahitaji ushauri wa Wanauchumi

Ninafanya kazi/kibarua sehemu fulani huku jiji la kanda ya ziwa

Nimepanga chumba nalipia Kodi 30k per month,.bill ya umeme na maji pia

Natumia nauli kwenda na kurudi kibaruani

Sasa nataka mwaka ujao nianze kuweka akiba Ila najiuliza kwa pesa hii nitaweza kusurvival mwezi mzima bila kukopa sehemu

Lengo langu nianze kutunza fedha kuanzia 2020 ,Sasa Wanauchumi nipeni mbinu za kufanikisha jambo hili kwa salary ya 120K

Asanteni
 
Mkuu hapo assume unalipwa 90000. Kwa hiyo ishi kwa bajet hiyo. Kodi ikiisha kapange karibu na kazini.

Utasave hela ya nauli. Pia ukiwa unafanya kaz tafuta kaz ya ziada baada ya saa kumi ufanye usirud home mapema.

Mazaga ya home uwe unanunua kwa ujumla.

Anyway hongera mkuu kwa kuishi kwa kipato hicho



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maamzi yako kwako uamue njia njia ya kusevu

hii ni mbinu ya kininja

Nenda mtandao wa simu unao tumia sajili line mpya halafu hiyo line utaongea na wenye mtandao wataifunga kwa muda unao taka wewe kusevu hela yako na kwa hiyo hela unayo pata unaweza kusevu


30,000 kila mwezi na ukaweka malengo ya kuwa ikifika kiasi fulan nitaenda kuifungua hiyo line

Ya pili u aweza kuwa unanunua vitu ambavyo unaweza kuja kuviuza baadae
 
Kodi 30 + umeme+maji+ nauli kwenda na kurudi.= 60,000 (nimechukulia nauli ni 400 kwenda na kurudi ndani ya siku 25).

Inabaki 60.
Chai 500*30=15000
Inabaki elfu 45.
Tuseme mchana usile uje ule jioni kwa budget ya 1500= 45000.
Hela imeisha . Hamna back ya kusave na bado itabidi mchana usile.

Jaribu kutafuta kazi nyingine zaidi. Usiitegemee hii tuu itakuumiza sana.
 
Back
Top Bottom