Msaada wandugu: Jinsi ya ku-bold maneno humu na WhatsApp

[Jini]
 
Kimsingi, kuna short cut za kuweka haya Maujanja, lakini kuna mahusiano ya moja kwa moja na elimu ya html.

Html inatumia tag, yaani tag za kufunga na kufungua.

Tag ni hizi:
[ ] Ya kuanza nayo, yaani mwanzo wa sentensi.
[/] Ya kumaliza nayo, yaani mwisho mwa sentesi.

Sasa basi, ndani ya hizo tag tunaweka alama ambazo zinawakilisha namna ambavyo tunataka neno letu liwe. Kumbuka hizo tag hutakiwi kuacha nafasi(kila tag ina alama hizi [ na ], so ninaposema hutakiwi kuacha nafasi, means itakuwa hivi: [])

Alama:
b inawakilisha wino wa moto, yaani bold

i inawakilisha mcharazo, yaani italic

u inawakilisha kupigia mstari, yaani underline.

color inawakilisha rangi, hapa kwenye rangi pia, ni lazima ujue jina la kiingereza la rangi husika.

Rangi:
[ color=blue ] Nataka rangi ya Buluu [ /color ].... Kumbuka ili itokee, hutakiwi kuacha nafasi, mimi nimeacha ili wewe uelewe.

Bold:
[ b ] Hapa nataka itokee bold [ /b ]

Italic:
[ i ] Hapa nataka itokee italic [ /i ]

Kumbuka: nimeacha nafasi ili uelewe, sasa kwa wewe ukitaka kujaribu husiache nafasi.

Ahsante.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…