Msaada: Wataalamu wa kilimo pitia humu

Msaada: Wataalamu wa kilimo pitia humu

Musaru

Member
Joined
Jul 5, 2015
Posts
38
Reaction score
24
Wadau habari, poleni na majukumu ya kazi na pia hongereni kwa kutoa elimu yenye ueledi juu ya masuala mbalimbali. Ninaleta mada kama ilivyotajwa hapo juu nikiamini nitapata majibu stahiki kwani jamii forum hasg jukwaa hili limesheheni watu wenye ujuzi na taaluma pia waliobobea katika nyanja mbalimbali.

Naombeni msaada wa michango yenu ya mawazo/hoja juu ya kilimo cha matikitimaji,mbali na mimi mwenyewe kuwa mkulima lakini huwa nalima kienyeji. Niko kwenye mchakato wa kulima aina hii ya matunda april 2016 ambapo utakuwa ni msimu wangu wa 8 lakini nataka kulima kitaalamu msimu ujao, sasa niko kwenye hatua za kati za kufanya tathmini za kiasi gani na gharama gani ya mbolea,viuatilifu(pesticides),mbegu pamoja na gharama zingine za uendeshaji.

Hivyo basi baada ya maelezo hayo hapo juu napenda kufahamu vitu vifuatavyo; 1.(a) katika eneo la ekari 1 ni kiasi gani cha lita za booster zinahitajika?

(inaendelelea hapa chini)
 
Inategemea na booster gani utakayoitumia, Application rate ya booster ndiyo itakayokusaidia kupata kiasi cha booster inayohitajika kwa ekari. Angalia kwenye karatasi ya maelekezo kisha ufanye mahesabu au uweke picha hapa tujue application rate yake tukusaidie kukokotoa kiasi kinachohitajika kwa eneo tajwa
 
1.(b) lita moja ya booster inatakiwa ichanganywe na lita ngapi za maji (c)boosting inatakiwa ifanyika mazao yanapofikia hatua ipi? 2.ni kiasi gani cha mbolea ya kupandia aina ya DAP kinatakiwa kiwekwe kwenye shimo moja litakalokuwa na miche miwili( shamba lina rutuba ya kawaida) 3.(a) ni aina gani ya viuatilifu inafaa zaidi kwa zao hili? (b)ni kiasi gani cha dawa kinatakiwa kwenye eneo la ekari moja?(c) je,kiasi hicho cha dawa kinatakiwa kichanganywe na lita ngapi za maji? NB; Katika kujihusisha kulima kwangu kienyeji huwa situmii mbolea na dawa ya aina yoyote hali inayopelekea kutopata matunda yenye ushindani sokoni ndio maana msimu ujao nataka kulima kitaalamu. Nakaribisha majibu,ushauri mashali na pia kukosolewa
 
Inategemea na booster gani utakayoitumia, Application rate ya booster ndiyo itakayokusaidia kupata kiasi cha booster inayohitajika kwa ekari. Angalia kwenye karatasi ya maelekezo kisha ufanye mahesabu au uweke picha hapa tujue application rate yake tukusaidie kukokotoa kiasi kinachohitajika kwa eneo tajwa

asante nashukuru ngoja nitaangalia kwenye karatasi hiyo,pia nitaiweka humu kwa ajili ya msaada zaidi.
 
Booster inategemea na zao pia range nyingi zinaanzia 50-60mls kwa lita 20za maji pitia vizuri maelezo kabla hujatumia
 
Booster inategemea na zao pia range nyingi zinaanzia 50-60mls kwa lita 20za maji pitia vizuri maelezo kabla hujatumia

Bab D naomba msaada km unajua hivi nao ufuta huwa unaweza kunyunyizia hiyo booster maana kuna mahari naandaa shamba nataka nilime kitaalam kdg
 
Kitaalamu kutumia booster ni sawa na kuamua kumlisha mtu asiye mgonjwa chakula kwa kutumia drip. Kikawaida mmea unatakiwa upate lishe yake kwa njia ya asili naayo ni kutoka udongoni. Hivyo unatakiwa kupata ushauri wa program ya mbolea kwaa ajili ya zao unalotakaa kulima. Ama kuhusu DAP na mbolea kwa ujumla kabla ya ushauri unatakiwa kufanya soil analysis ili kujua udongo wa shamba lako kama una ziada au upungufu kiasi gani ili kuweza kujua kiasi cha mbolea kinachoshauriwa. Kumbuka kuweka mbolea zaidi ya inayohitajika au pungufu kunaathiri mazao.
 
Vipo vitabu ambavyo vimeweka makadirio ya mbolea kimkoa lakini ni ''Blanket recommendation'' kwani ni vigumu kwa mkoa mzima kuwa na udongo na tabianchi yenye kufanana. Mbolea kama DAP huwekwa kabla ya kuotesha. Kwa mfano baada ya kutifua shamba unaweza kuweka DAP halafu ndio ukafanya harrowing ambapo mbolea itachanganyika na udongo. Baada ya hapo unaotesha.
 
Darasa zuri sana, nimependa watu wanavyochangia bila uchoyo wa elimu. mimi nililima matikiti ruvu mwaka jana nikapata faida kidogo, matikiti yanahitaji mtu awe na nafasi nzuri.
 
Bab D naomba msaada km unajua hivi nao ufuta huwa unaweza kunyunyizia hiyo booster maana kuna mahari naandaa shamba nataka nilime kitaalam kdg

Booster(ni mbolea ya majani inapigwa ktk majani) inatumika zaidi ktk mazao tete(high feeder crops) kwa ufuta tumia mbolea za chini
 
FOREVER LIVING
COMPANY
Je!! Kuna mtu unamfahamu
1. Anatafutampango kazi utakaomwezesha kustaafu miaka 5-10 akiwa na kipato maradufu?
2. Anatafuta njia ya kuongeza kipato cha ziada?
3. Ni mama na ungependa kukaa nyumbani na kulea watoto huku ukitengeneza kipato kizuri?
4. Ni mwanachuo unayetafuta njia mbadala ya kutafuta kipato kizuri?
Tuwasiliane; 0768 577 654
email; izackmanase@gmail
.com
fb : www.facebook.com//
Izack Manase
SAMBAZA UJUMBE HUU KWA WALENGWA UNAOWAFAHAMU. UWAOKOE NA UMASKINI ILI WATIMIZE NDOTO ZAO.

Unatuharibia thread zetu ww.
 
Booster inategemea na zao pia range nyingi zinaanzia 50-60mls kwa lita 20za maji pitia vizuri maelezo kabla hujatumia

Asante, nashukuru kwani umenipa mwanga, walau nimefahamu wapi pa kuanzia.
 
Back
Top Bottom