Msaada: Water Pump

1800

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2010
Posts
2,215
Reaction score
604
Wadau hasa wale wenye idea na water pump kwa ajili ya kilimo cha umuagiliaji wa kawaida,naombeni msaada wenu juu ya hizi water pump,hasa kuhusu bei,aina na uimara wake!hitaji langu kubwa kwa pump hizi ni kwa ajili ya kilimo cha bustani kama vile nyanya,pilipili mbuzi,carrot,nyanya chungu,pili pili hoho na vitunguu kama kuna uwezekano!nimeona kuna machine za kichina mpaka za 280,000/= lakini kwa kua sina uzoefu nikaona bora nije kwenu mnifungue macho!eneo nalotaka kulima ni la heka tatu,na umbali wa shamba mpaka mto ulipo ni kama mita 220 hivi!Natanguliza shukrani zangu!
 
ngoja kina Malila waje na mimi ninufaike
 

Hebu tembelea thread hii hapa chini ili upate mwanga kidogo kuhusu pump za umwagiliaji...

https://www.jamiiforums.com/ujasiriamali/387118-pump-za-maji-kwa-ajili-ya-umwagiliaji.html
 
waterpump kwa uwezo wako zitakufaa za kixhina ila unatakiwa uchukue yenye uwezo mkubwa kudogo maana mita 200 hiyo ya laki 2.5 haiwezi labda ununue tank uliweke jiran na chanzo cha maji halafu ulijengee juu kama kita nne hivi then utakuwa unasukuma maji kwenye tank halafu yanashuka by gravity kwwnye bustani yako. hii itarefusha maisha ya mashine yako. pia mashine itakuwa inatumia mafuta kidogo sana as compared kama utasukuma maji mita 200 . kwa uzoefu wangu mita 200 kuna kam pipa 3 hivi zitakuwa zinaielemea pampu yako hivyo kuongeza mzigo kwenye generator(engine)
 
Uko wapi mkuu,kama upo Dar au jirani na hapa jaribu kutembelea duka la autosokoni lipo mtaa wa India utapata pump yenye uwezo,uliyotaja hapo ni ndogo mno.unatakiwa upate pump yenye uwezo ili: (1)uitumie mda mrefu (2)Unakuwa na uwezekano kuongeza ekari bila kubadili pump.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…