Samboko
JF-Expert Member
- Oct 30, 2011
- 5,420
- 7,788
Naishi na mke wangu, tumejaaliwa kupata watoto mapacha wote wa kike wana umri wa mwaka na miezi 10, na bado wananyonya, Ni siku ya 3 sasa tangu mke wangu agundue ana ujauzito wa wiki 3, hatukupanga iwe hivyo lakini ndio imeshatokea.
Ushauri ninaoomba kwenu wataalamu na madokta waJF,
Mke wangu bado alikuwa ananyonyesha ila tangu ajue ni mjamzito amelazimika kusitisha kuwanyonyesha na maziwa yanajaa hadi yanauma, je nini kifanyike ili maziwa yasiendelee kujaa, na kuna madhara gani yanayoweza kumpata kwa kuacha kunyonyesha ghafla?
Je watoto watakua kwenye hatari yoyote kuwa karibu na mama yao na hali aliyonayo bila kudhurika? Na kama ndio, nini kifanyike ili wasidhurike?
Asanteni nawasilisha kwenu wakuu.