bhikola
JF-Expert Member
- Apr 2, 2012
- 1,131
- 1,663
Habari wanajamii.
Nimekuwa na shauku kubwa sana ya kuwekeza katika amana na dhamana hasa za serikali. Lakini nimekuwa nikipigwa danadana na watu wa kati ambao ni CRDB Bank.
Mwezi Januari nilitaka kununu dhamana. Nikamtumia mtu huyu wa kati maana nipo mkoani ambapo brokers wengine hawapo. Lakini kila wakati amekuwa akiniambia kuwa sishindi minada.
Sasa nashindwa kuelewa sishindi minada vipi? Akasema naweka bei ndogo. Nikaamua kuweka bei ya Tshs 100 kwa kila Tshs 100. Bado nikaambiwa sishindi. Hapa ndipo nilipogundua kuwa nahujumiwa.
Sasa nimeamua kumtafuta broker mwingine. Lakini changamoto ni kwamba, akaunti ya uwekezaji niliyofungua wanayo CRDB na hawataki kunipa jina na no za akaunti hiyo.
Nimejaribu kuwaandikia DSE kupitia ki barua pepe walichoweka pale kwenye tovuti yao nao hawataki kunijibu malalamiko yangu.
Nashindwa kuelewa, hamtaki watanzania tuwekeze kupitia hilo soko lenu au ni kitu gani hiki? Na je, Malalamiko yangu niyapeleke wapi?
Asanteni
Kama kuna sehemu inahitaji maelezo zaidi nipo tayari kueleza ili nisaidiwe