Msaada: Wazo la Biashara

vibatar

Member
Joined
Mar 16, 2014
Posts
57
Reaction score
16
Habari wana JF.

Msaada jamani ni biashara gani ambayo naweza kufanya nikaweza kuendesha life ikiwa nimepanga na mke na mtoto mmoja na nina msingi wa milioni mbili maana nawaza mapaka napagawa.

Asanteni! Naitaji ushauri wenu kwani hii milioni mbili nikama jicho kwangu na kama nikipoteza sijui itakuwaje kwani sina msaada wowote!

Asanteni.
 
Subiri waamke lakini tahadhari matapeli wamesikia hiyo m2 wataipigia hesabu kama yao,usikubali biashara yoyote ya Shea na mtu ushauri huo
 
inatosha kwa kuanzia lkn ni bora ukawa na shughuri ingine kwa ajili ya mambo ya kifamilia lkn ni tuambie yafuatayo, unaishi wapi ? ni mjini au kijijini? kwa sasa unafanya shughuri gani? hiyo 2m umeipataje? unaweza jibu hapa au pm
 
inatosha kwa kuanzia lkn ni bora ukawa na shughuri ingine kwa ajili ya mambo ya kifamilia lkn ni tuambie yafuatayo, unaishi wapi ? ni mjini au kijijini? kwa sasa unafanya shughuri gani? hiyo 2m umeipataje? unaweza jibu hapa au pm
 
Your business plan must focus the environment where you want to establish your business activities. Kwahiyo mipango iendane na mazingira uliopo. Asante
 
Mkuu umemuuliza maswali mazuri isipokua hilo alikopata hela naona kama is too confidential by the way ataamua ajibu au apotezee.

inatosha kwa kuanzia lkn ni bora ukawa na shughuri ingine kwa ajili ya mambo ya kifamilia lkn ni tuambie yafuatayo, unaishi wapi ? ni mjini au kijijini? kwa sasa unafanya shughuri gani? hiyo 2m umeipataje? unaweza jibu hapa au pm
 
Mkuu umemuuliza maswali mazuri isipokua hilo alikopata hela naona kama is too confidential by the way ataamua ajibu au apotezee.
haaaaa! kweli lkn lengo ni kutaka kujua ili iwe rahisi kumsaidia ndiyo maana nikamwambia anaweza pm au atakavyoona inafaa . nilitaka kuanza kumshauri kwa kuangalia aliwezaje kupata hiyo pesa pengine tunaweza boresha njia hiyo hiyo na akapata pesa zaidi.
na mara nyingi watu hufanikiwa kutokana na kufanya kazi walizo na uzoefu nazo . hicho ndicho kikanifanya kuuliza swali hilo
 

haina lengo bya mkuu,sasa mbona hajtokea tena!
 
Niliposoma mada nikasema nipitie ndani kuona waungwana wanamsaidiaje ndugu yetu alietueleza ni jinsi gani ana kiu ya kujiinua kutoka katika maisha fulani kuelekea mengine ila cha kushangaza watu naona wameanza zunguka sana kama vile wanataka mpa utaalamu ambao haupatikani popote zaidi ya kwenye akili zao tu. Okay nisiongee sana. Mkuu wazo zuri la biashara ni pale unapoangalia kwanza wewe unaweza fanya nini ktk jamii, unapenda nini, mtaani kwako kitu gani hakuna ambacho unaweza fanyia kama fursa ya kuanzisha kitu ambacho kitauzika na kuzalisha fedha yako, pia waweza fungua SimBanking kwa kuwa nimejaribu fuatilia line za uwakala TIGO kwenye laki 6 hivi, Airtel hadi laki na nusu au 2 na Mpesa pia 150 au 200. So kaa chini jifikirie wewe kitu gani waweza fanya then lete hapa watu wakusaidie zaidi ya hapo watu watakuzungusha kwa maswali yao ya kitaalamu na wasikupe chochote au pitia UZI wa ndugu yetu Chasha kama sikosei utaweza jifunza mengi. Asante.
 
Mkuu jaribu kuangalia katika sehemu unayoishi kuna mahitaji gani, kwa pesa hiyo ni vizuri ukapata vitu vinavyozunguka haraka haraka wala havili mtaji mkubwa;

Kwahio unaweza ukazunguka hapo mtaani au kwenye migahawa n.k. na kuuliza unaweza ukawa-supply nini iwe matunda, mazao hata mifugo. Ukishapata Order unaweza ukaenda sehemu vinavyopatikana hivyo vitu kwa bei rahisi. Kumbuka pia sometimes wewe mwenyewe ni mtaji tosha na kauli yako/uaminifu unaweza ukakufanya ukapewa mali kauli.., (yaani unapewa mzigo ukishauza mwisho wa siku unapeleka pesa).

Kuna watu wengi sana wanamizigo / bidhaa ila hawana soko, kwahio wewe kama una soko la lets say mbuzi unaweza kwenda kijijini au kuongea na watu hata kuwekesha bond ya kitu ili wakupe mali ukishauza uwape pesa yao na wewe kuchukua bond yako, au watu wenye mashamba ya mboga mboga unaweza kuingia nao contract ya kuwa unachukua mazao na kuwalipa mwisho wa wiki au mwisho wa mwezi. Kwa njia hizi unaweza ukajikuta unaanza biashara hata bila mtaji au kama una kadi ya gari au pikipiki unaweza kuitumia hiyo kama bond (sababu siku hizi wabongo hawaaminiki na kila mtu anaogopa kulizwa)
 
inatosha kwa kuanzia lkn ni bora ukawa na shughuri ingine kwa ajili ya mambo ya kifamilia lkn ni tuambie yafuatayo, unaishi wapi ? ni mjini au kijijini? kwa sasa unafanya shughuri gani? hiyo 2m umeipataje? unaweza jibu hapa au pm

Nipo dar kk! Nilikuwa na dizain viatu na kuuza mtaani lkn kwa sasa matilio ya kutengeneza hayazalishwi na hata yakizalishwa bei juu!..so hata km nikisema nitengeneze cwez pata faida...
 



Asante ndugu hat mie nilikuwa na wazo hilo nikajaribu kuuliza kwa mawakala wakanambia kwa sasa kupata lain ni shida hasa ya tigo kwan lain pekee lak 6 nainabidi niwekewe salio km la lak 4 niwe na lesen, na tin namba....! Hilo nikaona c tatizo so ndo plan 1 wapo iliyopo kwenye kichwa changu..alafu ndugu lesen inaweza kughalim bei gan! Asante
 



Asante ndugu
 
Tigopesa na m-pesa pia inategemea na eneo unalotegemea kufungua. Kama ni kariakoo baada ya miezi 6 wewe ni tajiri kaka maana huwezi kukosa laki 5 hadi 7 kwa mwezi, tena vile vibanda visiwe vingi sana ukibahatika uko pekeako itakua poa sana, ngoja nimualike Nkobe anaweza kutoa wazo zuri zaidi
 
Last edited by a moderator:
Ndizi toka mbeya?.
Mkungu 5000/2000000=mikungu 400.
Kuuza 10,000@mkungu=4000,000.
Transport 800,000.
Other cost 200,000.
Profit approx 1000,000 per each trip.
You do one trip per two week,there you got an income of 2000,000/= per month.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…