Mambo wanajamvi samahani kama nitakuwa nimekosea ila nahisi humu naweza pata njia ya kuniongoza.
Story fupi kuhusu mimi. Mimi ni mfugaji na changamoto napata kwenye chakula yaani nahitaji kutengeneza chakula changu kwa njia ya pellets sasa nauliza ni wapi nitapata mashine ndogo kwa bei chee ama humu kuna fundi wa kutengeneza?
Unauzoefu na ufugaji wa sungura na vyakula vyake? Sungura hawahitaji pellets kama samaki na kuku, sungura anakula karibu kila anachokula mbuzi, anapenda sana majani ya miti jamii ya miba kama mchongoma, mkungugu, lusina, shape ya majani jamii ya ukwaju hivii, mchunga (namba 1), mengine siyajui majina