Habari za wakati huu wanajukwaa,
Nina mdogo wangu kamaliza kidato cha nne Alipata ufaulu wa Division 2 na alisoma masomo ya Sanaa(arts) Kapata selection ya chuo cha uhasibu Dar es salaam (TIA) lakini kwa uchumi wangu sasaivi sijasimama kwaio itakua changamoto kidogo kumudu ada ya 890,000/= kwa mwaka .
HIVYO BASI:
Kama kuna mdau yeyote anafahamu Hatua za kufuata ili mdogo wangu apate shule ya serikali yeyote ndani hata nje ya Dar es salaam naomba anipe mwongozo tafadhari.
Natanguliza shukrani