Wanajamvi wenzangu mimi nipo kanda ya ziwa maeneo ya Muharamba Nkome Geita, kwa maeneo haya msimu wa mvua umeanza, ningependa mnijulishe ni mbegu ipi ya kitaalam itakayonifaa kwa kilimo na kama unayo maelezo machache ya kitaalam unielekeze. Natanguliza shukrani.