Mshobaa
JF-Expert Member
- Apr 7, 2013
- 1,714
- 677
Kwanza nianze kwa kutanguliza heshima mbele yenu, nina mdogo wangu ambaye huwa anasumbuliwa sana na kifua tangu akiwa na 2age mpaka sasa ana 12 age na bado tatizo linaonekana bado kuwa sugu kwani tumeshajaribu dawa karibia zote kwenye mahospitali na hakuna mafanikio yeyote, huwa anashinda vizuri ila ikifika saa moja jioni huwa anabanwa mpaka kupumua inakuwa ni tabu huku akikoroma kwa kuambatana na maumivu makali kifuani. Ombi langu kwenu kwa mwenye ufahamu wowote tafadhali tusaidiane kwa moyo mmoja... Dr Mzizi mkavu popote ulipo msaada wako hapa jamvini