Pole, ..Uzito wake na urefu ni upi?
Lakini unaposema ana tatizo la kifua una maanisha nini? ...anapumua haraka, anapumua kawaida ila kwa shida, ana pata maumivu kifuani, anakohoa au tatizo hasa ni lipi?
Tatozo hili humpata mara ngapi kwa siku/wiki/mwezi? Hutokea hasa wakati gani wa siku mf asb/mchana/usk? wakati gani wa majira ta mwaka wakati wa masika/kipupwe n.k! Je kuna dawa zozote kati ya zile alizowahi kutumia ziliwahi kumpa unafuu? Zipi? Tofauti na kifua je, mtoto husumbuliwa na harufu ya marashi, baadhi ya viungo!!
Vipi tatizo la kutokwa jasho jingi, mikono (hasa vidole vya miguu kubadilika na kuwa kama rangi ya blue), choo chake kikoje (kilicho laini sana)?Kuna mtu katika familia/ukoo mwenye tatizo kama hilo?