msaada wenu unahitajia tafadhali..!!

msaada wenu unahitajia tafadhali..!!

mitutwe pazi

Senior Member
Joined
Feb 16, 2013
Posts
150
Reaction score
28
Habari za jioni wakuu...ni matumaini yangu weekend iko poa kwa upande wenu.
kuna suala moja la kisheria ambalo ningependa kuomba msaada wenu, suala lenyewe ni kama ifuatavyo

kuna bro wangu ambaye amenunua kiwanja, lakini manunuzi yenyewe ya kiwanja yamefanyika kindugu sana kiasi hakukuwa na ushirikishwaji wa mamlaka yoyote ya serikali kama mjumbe au serikali za mitaa, na hii yote ni kwa sababu ameuziwa na mtu wanaefahamiana kwa ukaribu sana.

kama mnavyofahamu mazingira ya uaminifu si mazuri sana hususani katika kipindi hiki cha demand kubwa za maeneo, hivyo naomba kufahamu ni njia gani za kisheria ambazo anaweza kuzifuata ili kuweza kupata hati ambayo itaonyesha kama yeye ndio mmliki halali wa kiwanja husika.

Natanguliza shukrani..
 
Pole sana ndugu! Km unavyojua sheria lazima ifuatwe, na mauziano hayo yanatakiwa yathibitishwe na mkataba wa maandishi na kwa maana hiyo mauziano ya viwanja yantakiwa yafuate msharti ya kanuni za ununuzi km inavyoelezwa na sheria ya ardhi sura no.113 !
Sasa swala la kupta hati miliki inatakiwa mauziano hayo yawe kwa misingi ya sheria km nilivyokueleza! Sasa kinyume na haoo sidhani km kuna njia maalumu na ya kisheria ya kuweza kupata hiyo hati!
I stand to be corrected! Otherwise I submit!!
 
Back
Top Bottom