Pole Uzuri...ukifuatilia thread yenye kichwa kinachosema 'ERYTHROPOETIN 4000IU SC Dawa ya FIGO' utakuta comment zinazojibu swali lako.
Mafigo kwa kawaida huwa yanatoa kichocheo kinachoitwa 'Erythropoietin', hiki kichocheo hustimulate bone marrow kuzalisha chembe chembe nyekundu za damu (red blood cells). Mafigo yanaposhindwa kufanya kazi (mafigo yote mawili, maana figo moja inatosha kufanya kazi za figo mbili katika mwili wa binadamu) basi hiki kichocheo hakitolewi, na hivyo bone marrow haizalishi red blood cells inavyotakiwa. Hii inasababisha mgonjwa kupungukiwa na damu mara kwa mara na kulazimika kuongezewa kwani hata akimeza dawa za kuongeza damu hazitamsaidia.
Kwa hiyo kama vipimo vikithibitisha bone marrow inafanya kazi (bone marrow aspiration/biopsy), basi mgonjwa atahitaji apate sindano za Erythropoietin ili bone marrow ziendelee kuzalisha red blood cells na mgonjwa asipate upungufu wa damu.