Jamani umekuwa ikinitokea Mara kwa mara kwa kipindi hiki.
Hapo mwanzo nilikua nakunywa pombe nyingi sana bila madhara yeyote ,pia nilikua napendelea pombe kali.
Lakini hali imebadilika kwa sasa nikinywa tu kesho yake nitashinda nimelala na tumbo linauma. Pia lazima nijitapishe ili kutoa nyongo ili nipate ham ya chakula. Lakini katika kutapika natapika na damu hii ndio hunitisha zaidi
Wana jamvi kutapika damu nini sababu na je kunamadhara gani yanayoninyemelea
Tiba ipi nipate?
Napenda kuacha pombe ila ni ngumu sana.
Masikiniiii...nakuhurumia ndg yangu...karibu pm nikusaidie...nimefanikiwa kupiga chini mitungi enselevu kwa 6 yrs now...naweza kukupa mbinu za kuacha ila kwa uwezo na msaada wa mungu utafanikiwa.
Nje ya mada...
Huwa nasikitika sana, pindi ninapo ona tunaelekea kumpoteza mpendwa wetu, mwenzetu ama rafiki yetu, kwasababu ambazo zinaweza kuzuilika ama uzembe.