Kwanza niseme, Ashakum si matusi. KUNDULE ni neno linalotokana na neno ----- na kiangami (clitic) LE kinachotokana na LAKE. Mfano mwingine wa kiangami ni MAMAKO (mama + yako). Neno ----- hasa linatokana na ------. Kuondoa kiambishi M- kunafanya nomino hiyo iwe kubwa kwa maana ya kuikuza.
Hadithi yenyewe ni kwamba nyani ana makalio yanayochekesha kwa nyani wenzie. Lakini mwenyewe haoni kwamba yuko hivyo pia. Naye anawecheka wengine.