habari wana jf,naomba kujua dawa ya kusafisha mkojo nahisi mkojo wangu mchafu kwa dalili hizi,maumivu wakati wa kukojoa,mkojo unatoa harufu sana,rangi ya mkojo kama kutu nimejaribu kunywa maji mengi sijafanikiwa

Pole sana. Mimi sio daktari na huu ni ushauri wangu kwako kwa experience yangu binafsi. Ushauri huu utakufaa zaidi kama wewe ni mwanaume kwa sababu mimi pia ni mme. Cha muhimu sana nenda kapime mkojo wako kwa kipimo kinaitwa urine urinalysis (sina uhakika kama hizi ndo spelling zake) baada ya hapo kama mkojo wako una infection watakuambia na kukuandikia dawa. Kama hawataona tatizo basi ni vizuri ufanye culture. Culture kwa kifupi ni uchambuzi zaidi wa mkojo kwa kuoteshwa halafu baada ya siku tatu watakupa jibu kama kweli una infection au la. kama hawatapata kitu chochote basi nakushauri ukamwone dakatari mtaalam wa mkojo anaeitwa urologist. Huyu daktari mtaalam atakuambia kama ni infection kwenye figo au labda ni infection kwenye prostatitis (yanapozalishwa manii) Mwisho mkuu usimeze dawa bila kucheck mkojo wako kama una infection. Na zaidi endelea kunywa maji mengi na usibane mkojo. Ukisikia kwenda haja ndogo nenda mara moja.