mamayeyoo
Member
- Dec 27, 2013
- 86
- 22
Anaitwa mwanaisa. Ni binti mwenye umri wa miaka 21. Alikulia katika kijiji kimoja huko Moshi. Alisoma mpaka kidato cha tatu lakin kwa bahati mbaya wazazi wake walishindwa kulipa ada ya mtoto wao baada ya kufilisika. Lakini alikuja jijini Dar es salaam kwa dada yake. Dada yake alijitahidi kumtafutia shule lakini baadae pia alishindwa kulips ada kutokana na ugumu wa maisha. Binti yule alifanya kazi ya kuchambua mawe ili aweze kusoma elimu ya watu wazima lakini hela haikutosha kutokana na hela kutumika katika matumizi ya nyumbani.basi alikaa bila kazi kwa muda mrefu baadae akapata mama ntilie na kufanikiwa kujiandikisha (QT). Amesoma mpaka mpaka sasa form four lakini ameshindwa kulipa ada na imebaki miezi michache amalize kidato cha nne. Kwa yoyote atakayeweza kumsaidia binti huyu kwa moyo tafadhali msaidie amalize masomo yake.