Msafara wa Viongozi CHADEMA wazuiliwa kuingia Uwanja wa Uhuru kumuaga Mzee Mkapa. Waitaka Serikali itoe maelezo...

Sasa mbona walijiwahi kwenda Taifa?

Kwanza hata niliposikia hao viongozi wa Cdm wameenda niliwashangaa. Unaendaje kwenye msiba wa kiongozi ambaye maisha yake yote alikuwa adui, na muendesha siasa za ufitini dhidi ya upinzani, hasa hasa hao cdm? Huyo Mkapa si alimuweka ndani kabisa huyo Lisu wakati akipambania wachimbaji wadogo?
 
Unajuaje walichelewa, weka picha na timer.
 
Kwa Mara ya kwanza katika historia ya Tanzania utawala wa magufuli umekuwa wa kwanza kutugawa watanzania kwenye misiba Yani wametoa ujumbe tusizikane asanteni CCM.
 
Kwani baada ya kuingia rais wananchi hawaruhusi kuingia nyuma yake?
mwananchi wa kawaida anaruhusiwa kimya kimya kuingia

huo msafara sio wa wananchi wa kawaida na kama undhani kina

mbowe,lissu,mnyika,Full team nzima ni wananchi wa kawaida,sawa lalamika.
 
 
Je, walienda kwa dhania ya Kumuaga Rais Mstaafu Hayati Mzee Mkapa au walienda ili Kujitangaza zaidi Kisiasa na Kumuonyesha Mgeni Mwenyeji?
Tunapimaje DHAMIRA za watu kwenye hili? Huu ni msiba wa Rais Mstaafu!
 
Kwani kwenda msibani unapangiwa muda ? Haya mambo ni ya ajabu
Swala la msiba halina uhusiano na protokali hio sio siasa.......ccm na viongozi wake waache utoto huu......

Wanazuiaje watu kuingia msibani? Pathetic
 
Hawakujua siku ya leo ilikuwa ni shughulia ya mazishi ya kitaifa. Shughuli ya kitaifa ina protokali maalumu ya kuingia uwanjani . Walitakiwa kuingia wakati wa zamu za viongozi wa kisiasa kama walivyofanya wenzao. Au wawahi saa kumi na mbili waingie kama wananchi wa kawaida. Prorokali ya leo kiongozi wa mwisho kuingia alikuwa Rais na ratiba kuanza si vinginevyo.
 
Je walifuata mambo ya itifaki? Maana wasifanye kama msiba wa mtu wa kawaida.
Mtu akisimama nje ya mlango wa choo huwezi kujua kama anaenda kunya au kukojoa
 
Kwa jinsi walivyojikusanya na kwenda Uwanja wa Taifa, ni wazi kabisa walitaka kick ya kisiasa, sasa hao walikuwa hawana nia ya kuhani msiba bali kujitangaza kisiasa na wangevuruga sana..
Msiba mkubwa wa Taifa na Kimataifa kama huu wa Mh. Mkapa, alafu unakuja na sura au mlengo wa kisiasa ili ujipatie kick au publicity ni mbaya sana, watu wako katika majonzi ww uje na magwanda yako ya CDM unatafuta nn? 🤔😠 Alafu wanakuja Mh. Rais tayari yuko ndani ya Uwanja wa Taifa, hata hawajui itifaki, hii ni kosa.
 
Mbona nyie mmejaa na minguo yenu ya mbogamboga kwani hamkuwa mnatafuta Kiki za kisiasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…