Tatizo hujawa specific,ni kiongozi yupi,magari ya kifahari yapi(maana kila mtu ana vipimo vyake vya magari ya kifahari).Kwa viongozi kama Rais,Makamu wake au waziri mkuu hizo ni taratibu za kawaida kabisa za ulinzi.Kama unakumbuka tulivyompoteza Sokoine,lawama zilienda kwa wanausalama,sababu ya Escort chache zilizopelekea gari ya waziri mkuu kugonga gari ambayo haikuwa kwenye msafara.Asubuhi ya leo nikiwa mbele ya kituo cha Polisi Salendar Bridge ulipita msafara wa kiongozi mmoja wa juu serikalini anaenda zake ofisini ulikuwa msusururu wa magari ya kifahari yapatayo sita na pikipiki,Sasa nikajiuliza msafara ni kwa ajili ya wanausalama tuu au ni ufahari fulani?Wana JF nisaidieni hapa.
Hakuna maelezo ya maana zaidi ya uzembe unaosababishwa,ama na mawasiliano mabaya kati ya Usalama wa taifa na police,lakini nachoelewa ratiba ya kiongozi mkubwa hutolewa mapema kwa Rpc wa eneo husika,sasa utakuta uoga wa askari wa usalama barabarani wanasimamisha magari mapema wasiharibikiwe na kazi,na kumbuka amri ya kusafisha njia inatoka kwa RTO(Region Traffic Officer) kupitia Radiocall,ambaye gari yake inakuwa mbele kwenye msafara ikisafisha njia.Au unaweza kuta ni sababu za kiusalama kwa siku ile.Duh hapa ningempata wa kunipa maelezo kamili ningefurahia sana
Mi naonaga kama kero. Kuna siku Tulisimamishwa ile kona ya kutokea Ikulu
Kwa muda wa nusu saa ndo msafara unapita. Nilijiuliza maswali Mengia sana
yasiyokua na majibu.