BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,165
Waziri Wassira apigwa mawe
Magari ya viongozi waliofuatana naye yapasuliwa vioo
na Berensi Alikadi, Bunda
Tanzania Daima~Sauti ya Watu
JESHI la Polisi wilayani hapa, linawashikilia watu 11 kwa tuhuma za kuupopoa kwa mawe msafara wa viongozi wa wilaya, akiwamo Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wassira.
Tukio hilo lililosababisha magari kadhaa kupasuliwa vioo, lilitokea juzi wakati msafara wa viongozi hao ukitokea katika sherehe za kuuaga mwaka 2008 na kuukaribisha mwaka mpya wa 2009, huku gari la Waziri Wassira likinusurika baada ya kupita kwa kasi eneo hilo.
Tukio hilo lilitokea juzi, majira ya saa sita usiku wakati viongozi hao wakirudi majumbani mwao, wakitokea katika ukumbi wa Chuo cha Ualimu Bunda, kulikofanyika sherehe hizo, zilizokuwa zimeandaliwa na mkuu wa wilaya na kuhudhuriwa na Waziri Wassira, ambaye alikuwa mgeni rasmi.
Viongozi hao walikumbana na zahama hiyo mara baada ya kufika eneo la Nyasura, ambapo walikutana na kundi kubwa la vijana waliokuwa wakisherehekea kuupokea mwaka mpya.
Kama vile waliamrishwa na mtu, baada ya kuona msafara huo, vijana hao kwa nyakati tofauti kila mmoja alitafuta jiwe na kuanza kuyatupia magari hayo, huku wakiuita msafara huo kuwa ni wa mafisadi.
Magari yaliyopondwa mawe na kuvunjiwa vioo ni la Mamlaka ya Maji mjini hapa, lenye namba DFP 1949, aina ya Toyota Land Cruiser na SM 2986 Toyota Land Cruiser, ambalo lilikuwa limewabeba viongozi wa mji huu, kwa ajili ya kuwarudisha makwao.
Magari mengine ni pamoja la Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri, SM 4225, la Katibu Tawala, STJ 2884, ambalo lilipasuliwa kioo wakati likiwa limetoka kumsindikiza Waziri Wassira nyumbani kwake.
Gari jingine lililokumbana na mkasa huo ni lenye namba za usajili T 694 ADJ, linalomilikiwa na Hospitali Teule ya DDH.
Aidha, vijana hao licha ya kulirushia mawe gari la Waziri Wassira, hawakuweza kulisababishia uharibifu, kwani lilipita kasi katika eneo hilo, ambapo nyuma yake, lilikuwa likifuatiwa na gari la wanahabari.
Wengine waliopigwa mawe na kundi hilo la vijana ni pamoja na muuguzi wilayani hapa, Nelson Malisa, ambaye alikuwa akiendesha pikipiki aina ya Toyo na Mwenyekiti wa Mtaa wa Migungani, Simon Mwita, ambaye amejeruhiwa na kulazwa katika Hospitali ya DDH .
Kwa mujibu wa polisi, watuhumiwa hao watawafikisha mahakamani muda wowote kujibu tuhuma zinazowakabili.