KOKUTONA
JF-Expert Member
- Jan 29, 2011
- 8,651
- 6,104
Hodi humu.
Juzi nilikuwa kwenye dala dala, na ilikuwa imejaa sana. Bahati mbaya mkaka mmoja alimkanyaga mdada kwa bahati mbaya. Yule mdada akaja juu kweli, lakini yule mkaka akajishusha akaseme na kumuomba radhi yule mdada. Nanukuu "Samahani dada, sikudhamiria kukukanyaga, pole sana. Ndo hivyo tena MSAFIRI KAFIRI"
Mara watu waaanza kunong'ona chini chini, akatokea mdada mmoja akasema "Kaka unatuharibia lugha bwana hakuna kitu kama,msafiri kafiri ni MSAFIRI KAKIRI"
Yalianza mabishano ya pande mbili, yaani wanaoamini kuwa sahihi ni msafiri kafiri na wanaojua sahihi ni msafiri kakiri.
Nilishuka mabishano yakiwa yanaendelea, na habari ya dada kukanyagwa iliyeyuka ghafla.
Wataalam wa lugha naomba kujuzwa, ipi ni sahihi? Kwa uelewa wangu siku zote nilikuwa najua msafiri kafiri, hii kakiri ilikuwa mpya kwangu.
Nawasilisha