kwanza ni wape pole sana ndo mambo ya dunia hii hasa kwa watu wasokuwa na hofu ya mungu.
kisheria mgao upo kwenu nyote kama watoto na warithi halali wa mali ya marehemu. kwa mhujibu wa sheria za mirathi katika nchi hii kuna mirathi
1.palipo na wosia
2.pasipo na wosia
wosia waweza kuwa wa maandishi au bila kuandikwa.
Sheria za mirathi itumikayo Tanzania imegawanyika katika sehemu tatu:-
i) Sheria ya Urithi ya India1865.
ii) Sheria ya Kiislamu.
iii) Sheria ya Kimila.
bila shaka kama umesema marehemu alifunga ndoa manake alikuwa mkristo na sheria inayoweza kutumika hapo kwa kuzingatia vigezo vingine,ni Sheria ya Urithi ya India 1865.
katika sheria hii utaratibu wa mgao ni kama ifuatavyo,
1.Kama marehemu ameacha mjane na watoto watapata kama ifuatavyo; mjane1/3 na watoto 2/3 ya mali yote ya marehemu ambayo hugawiwa sawasawa.
2.Kama marehemu hakaucha watoto , mjane atapata ½ na ½ nyingine hugawanywa sawasawa kati ya wazazi , kaka na dada za marehemu.
Zingatia: Kwa mujibu wa sheria hii watoto wa nje ya ndoa hawana haki ya kurithi isipokuwa kama kuna wosia na katika wosia huo wawe wamerithishwa mali.
umesema kuwa mlimchagua mama yenu kama msimizi wa mali ya marehemu (mirathi), kimsingi alitakiwa kuthibitishwa na mahakama yenye mamalaka katika eneo mlipo hapa nazungumzia mahakama ya mwanzo ya eneo husika,
kwa mujibu wa sheri hii kazi za msimamizi wa mirathi ni kama ifuatavyo
WAJIBU WA MSIMAMIZI WA MIRATHI.
Ndani ya miezi 6 baada ya kuteuliwa kuwa msimamizi wa mirathi , msimamizi anawajibika kutoa orodha na kiasi cha mali alizoacha marehemu, fedha taslimu, madeni pamoja na idadi ya marehemu anaotegemea kuwagawia mali za marehemu.
Kukusanya kwa uaminifu mali za marehemu.
Kuorodhesha madeni yalioachwa na marehemu pamoja na kuyalipa madeni hayo toka kwenye mali alizoacha.
Kulipa gharama za mazishi na gharama za kuendesha mirathi toka kwenye mali za marehemu.
Kugawa mali za marehemu kwa warithi halali kama marehemu atakuwa ameacha wosia msimamizi atagawa kufuatana na wosia aliondika marehemu na kama hakuna wosia atagawa kulinganba na sheria inayotumika kwenye mirtahi9sheria ya kimila, kiislamu, au sheria ya mirtahi ya India.
Kushtaki ambapo marehemu angeshtaki ili kudai haki zake au kujibu mashitaka ya madai pale ambapo kutakuwepo na madai dhidi ya msimamizi.
Kusikiliza maelezo yanayotolewa na mahakama kuhusiana na mirathi anayoendesha.
Kutoa taarifa mahakamani inayoeleza alivyoendesha mirathi na kugawa mali kwa warithi wa marehemu na hatimaye mirathi kufungwa.
NINI UFANYE SASA.
Kama utakuwa umenielewa kidogo,juu ya haki zenu wote bila kujali jinsia zenu pamoja na mama yenu,unaweza kwenda mahakamani wewe mwenyewe au kwa msaada wa watu unaoamini wanaweza kukusaidia,ili kuiomba mahakama imlazimishe mama huyo kugawa mali hizo kwa warithi wote wa marehemu.
samahani nimeandika kirefu kidogo kwakuwa suala hili limeonekana kusumbua jamii yetu kwa kiasi kikubwa sana.
.