Msahama wa wafungwa kwenye sherehe ya uhuru hauhusu wa jinsia ya kike?

Msahama wa wafungwa kwenye sherehe ya uhuru hauhusu wa jinsia ya kike?

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2012
Posts
13,171
Reaction score
23,996
Nimejaribu kuangalia majina na video za wafungwa katika baadhi ya magereza nchini waliopata msamaha wa Rais Magufuli katika sherehe za Uhuru wa Tanganyika lakini kitu kinachonifanya nishangae ni kukosekana kwa wafungwa wa kike!

Je, Tanzania hakuna wafungwa wa kike? Kama wapo, kwa nini hawaonekani katika makundi ya wafungwa waliopata msamaha kisheria?

Je, Hii inadhihirisha watu wanaofanya uhalifu nchini na kufungwa jera ni jinsia ya kiume pekee? Kwa nini jinsia ya kike haifungwi gerezani?

Je, Hii inadhihirisha kuwa Tanzania bado kuna mfumo dume kwa maana kuwa jamii ya kike haina sauti na kutokuwa na sauti kunawafanya wao ni wahanga (victim) katika jamii?
BAADHI YA VIDEO:

 
MOD'S naomba mnisaidie kubadilisha kichwa cha mada, badala ya kuandika ''msamaha'' nimeandika ''msahama''

Natanguliza shukrani zangu!
 
Mbona kwenye hii video nimeona pembeni kushoto mwa huyo mwachiliwa aliyekuwa anazungumza kwa niaba ya wenzake..
Kushoto kwake kuna mdada kichwa chake kinaonekana kasuka twende kilioni..
Huyo nae kaachiwa huru.
Angalia vzr utaona.
 
Wanawake ni asilimia ndogo sana ya wafungwa wote gerezani, nadhani hata 10% hawafiki, so haistaajabishi sana kutowaona

Pia kuna vile vigezo vya msamaha alivyotoa Rais ambavyo mfungwa anatakiwa awe amebakisha chini ya mwaka mmoja wa kifungo chake, so wanawake wengi inawezekana hawajafikia hicho kigezo, na haishangazi sababu wapo wachache sana
 
Kati ya wafungwa wote Tanzania sijui kama wanawake wanafika hata elfu moja. Hivyo watakaonufaika na msamaha pia watakuwa wachache sana.
 
Kati ya wafungwa wote Tanzania sijui kama wanawake wanafika hata elfu moja. Hivyo watakaonufaika na msamaha pia watakuwa wachache sana.
Mleta mada kiboko anataka usawa Hadi wa kufungwa gerezani anataka idadi ya wanawake iwe sawa na wanaume
 
Back
Top Bottom