Detective J
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 30,742
- 56,070
Alipatikana mmoja amepigwa pini, wananchi wenyewe ndio wanatakiwa waonyeshe msimamoCcm is there forever Mpaka wapatikane wapinzani ambao hawapo katika Payroll ya Ccm na sio hawa akina naninalii
Kibarua wa Komredi Polepole hujambo? π
Waliomuona jana kwenye kongamano wanasema kachoka na uso hauna nuru! Sura imesawajika na anaonekana dhaifu na dhoofu! Haya si maneno yangu bali ya waliomuona
Kwenye Biblia takatifu kitabu cha Mithali kuna mstari unasema .. HERI MEKO KAVU PAMOJA NA UTULIVU....!
Hakuna kitu kinamaliza watu kama midomo ya wengine! Macho ya wengine! Vidole vya wengine...!
Wakinyanyua vinywa hata kama hawakusemi wewe tayari kuna matamshi yanajiumba na kudhani yamekulenga wewe. Unajikuta unakosa raha!
Macho! Hakuna taa ina mwanga mkali kuzidi macho! Yakikuangalia utadhani yanakuona mpaka rohoni... Utadhani yana x-ray.. Halafu yanasengenya vibaya Sana!
Yanakusema
Yanakuonya
Yanakuhukumu
Yanakukebehi
Yanakufanyia kila aina ya michezo hasa ukiwa mbele ya kadamnasi..
Vidole: havina midomo wale macho lakini vina ishara! Mdomo ukisema, macho yakikuangalia unapata hisia na vidole vinakunyooshea
Unajikuta unakosa amani, unakosa furaha unakosa confidence.. Kwakuwa unadhani kuna walio nyuma yako wanakunyooshea vidole!
Hapa tulipofika! Haina comeback! Maana
Midomo inayocheza cheza inazidi kuongezeka kila uchao.
Macho yanazidi kupata nuru
Vidole vinazidi kuwa virefu
Ni tafrani kila kona! Huna muda wa kuchill tena wala kutabasamu.. Si mitandaoni si vijiweni si mafichoni.. Hata kama huwasikii na kuwaona lakini kina hisia zinakuambia kwamba wanakusema
Msaidieni apumzike kwa amani.. Ameshatukanwa mpaka matusi ambayo haya andikiki.. Ameshapewa kejeli za kila aina! Dhihaka na hata tuhuma zenye ithibati
Kama binadamu mwenye hisia
Kama binadamu mwenye familia
Kama binadamu mwenye ndugu jamaa na marafiki haya mambo yanaumiza Sana
Msaidieni apumzike.. Apumzishe hisia
Naye anahitaji faraja
Naye anahitaji heshima
Naye anahitaji kutambuliwa utu wake
Lakini je naye kayafanya haya kwa wengine!? Kwakuwa ukitenda wema utalipwa na ukitenda ubaya utalipwa ubaya!
Karma is bitch! Huwezi Ku panda ukwaju ukategemea kuvuna bangiView attachment 3452164
Mshana Jr naona anautaka huyu.Kibarua wa Komredi Polepole hujambo? π
nawe yanakuhusu kuwa mpinzani wa kweli. nani kama siyo wewe na mimi? Unamtegemea nani? You are part and parcel of the responsibilityCcm is there forever Mpaka wapatikane wapinzani ambao hawapo katika Payroll ya Ccm na sio hawa akina naninalii
Hapa Kalenga mgombea wetu hana mpinzani kwa hiyo tunasherehekea tu hadi siku ya kutangazwa na mkurugenzi October ππIna hang'over ya visungura halafu haina hela ya supu .
Hawa walionunuliwa na lowasa 2015.Ccm is there forever Mpaka wapatikane wapinzani ambao hawapo katika Payroll ya Ccm na sio hawa akina naninalii
Tuichangie tu isije ikatufia bure.Tuichangie ama tuipotezeeπ
Sio 2015 tangia 1992 hamna upinzaniHawa walionunuliwa na lowasa 2015.
Polepole aliingia na maburungutu ya fedhs kuwachangia faini ya kuwatoa Jela Mwenyekiti Mbowe na Katibu mkuu Dr MashinjiTuichangie ama tuipotezeeπ
Jipangeni Leo ni Askofu Gwajima ππTuichangie tu isije ikatufia bure.
Leo Gwajima kesho Mpina muwe erna MB za kutosha ππMit 17
1Afadhali mego kavu pamoja na utulivu,
Kuliko nyumba yenye karamu nyingi pamoja na magomvi.
2Mtumwa atendaye kwa busara atamtawala mwana atendaye mambo ya aibu;
Tena atapata sehemu ya urithi kati ya ndugu.
3 Kalibuni kwa fedha, na tanuru kwa dhahabu;
Bali BWANA huijaribu mioyo.
4Mtenda mabaya husikiliza midomo ya uovu;
Na mwongo hutega sikio lake kusikiliza ulimi wa madhara.
5 Amdhihakiye maskini humsuta Muumba wake;
Naye aufurahiaye msiba hatakosa adhabu.
6Wana wa wana ndio taji ya wazee,
Na utukufu wa watoto ni baba zao.
7Maneno mazuri hayapendezi kinywani mwa mpumbavu;
Siuze midomo ya uongo kinywani mwa mkuu.
8 Kipawa ni kama kito cha thamani machoni pake yeye aliye nacho;
Kila kigeukapo hufanikiwa.
9Afunikaye kosa hutafuta kupendwa;
Bali yeye akashifuye neno hutenga rafiki.
10Lawama hupenya moyoni mwa mwenye ufahamu,
Kuliko mapigo mia moyoni mwa mpumbavu.
11Mtu mwovu hataki neno ila kuasi tu;
Kwa hiyo mjumbe mkali atatumwa kwake.
12Afadhali mtu akutwe na dubu aliyenyangβanywa watoto wake,
Kuliko na mpumbavu katika upumbavu wake.
13 Yeye arudishaye mabaya badala ya mema,
Mabaya hayataondoka nyumbani mwake.
14 Mwanzo wa ugomvi ni kama kutoboa penye maji;
Basi acheni ugomvi kabla haujafurika.
15 Yeye asemaye kwamba asiye haki ana haki;
naye asemaye kwamba mwenye haki hana haki;
Hao wote wawili ni chukizo kwa BWANA.
16Nini maana yake, mpumbavu kuwa na fedha mkononi mwake ya kununulia hekima,
Ikiwa hana moyo wa ufahamu?
17Rafiki hupenda sikuzote;
Na ndugu amezaliwa kwa siku ya taabu.
18Aliyepungukiwa na akili hupana mkono na mtu;
Na kuwa mdhamini mbele ya mwenzake.
19Apendaye ugomvi hupenda dhambi;
Auinuaye sana mlango wake hutafuta uharibifu.
20Mtu mwenye moyo wa ukaidi hatapata mema;
Na mwenye ulimi wa upotofu huanguka katika misiba.
21Azaaye mpumbavu ni kwa huzuni yake mwenyewe;
Wala baba wa mpumbavu hana furaha.
22Moyo uliochangamka ni dawa nzuri;
Bali roho iliyopondeka huikausha mifupa.
23 Asiye haki hutoa rushwa kifuani,
Ili kuzipotosha njia za hukumu.
24 Hekima huwa machoni pake mwenye ufahamu;
Bali macho ya mpumbavu huwa katika ncha za dunia.
25Mwana mpumbavu ni huzuni kwa babaye,
Na uchungu kwa mamaye aliyemzaa.
26Tena kumwadhibu mwenye haki si vizuri;
Wala si kwema kuwapiga wakuu kwa unyofu wao.
27 Azuiaye maneno yake ni mwenye maarifa;
Na mwenye roho ya utulivu ana busara.
28Hata mpumbavu akinyamaza, huhesabiwa hekima;
Akifumba midomo yake, huhesabiwa ufahamu.....
View attachment 3452181
Kala Ushahidi wa Siri πβοΈMla jana kala nini.. !