JF DOCTORS msaada wenu unahitajika sana, Kuna jamaa yangu mmoja anasumbuliwa na vitu viwili
1) Huwa anawashwa bila sababu, hana upele, ila akiwa anajikuna vile vipele vya kuku vinatokeza vingi. baadae muwasho unapoa vipele vinatoweka. anamuda sasa tangu aanze kupata matatizo hayo.
2) Alianza kukohoa tangu Mwezi wa pili trh 10, mpaka leo hajapona na huwa akihema kwa nguvu mapafo au kwenye koo kuna unguruma, ametumia dawa zote muhimu za kawaida za kifua lakini bado hazijasaidia.
NASUBIRI MAONI YENU WANA JF
1.MWANAUME AU MWANAMKE? 2.UMRI 3.YUPO MKOA GANI 3.SEHEMU HASA YA MUWASHO [MAUNGIO.MWILI MZIMA AU WAPI?]4.KIFUA KILIANZA SAMBAMBA NA KIKOHOZI AU?KIPI KILITANGULIA5. VIPELE VYA KUKU?[UNAMAANANISHA NINI,SEHEMU GANI YA KUKU YENYE HUO MFANO e.x.mdomo,mguu?]6.kwao kuna wagonjwa wa kifua ex.pumu n.k?7.NI AKIWA KATIKA MAZINGIRA GANI NDIO TATIZO LINAANZA[NYUMBANI KAZINI,SHAMBANI],JE MUWASHO UKIANZA HUAMBATANA NA MAFUA[CHAFYA,KUWASHA MACHO NA MACHOZI AU KIOH ZI?].
Dawa gani alitumia?
Mara nyingi miinuko hiyo[burrows] huonekana zaidi kwenye vidole au katikati yake.,juu ya viganja,katika maungio ya mikono [ elbow ] ,kwenye maumbile ya [male genitalia] kwenye kiuno sehemu ya mzunguko wa mkanda na chini ya ******.Michirizi ya kwenye ngozi sababu ya kujikuna.Kama hizo barrows zitakuwa sehemu za wazi kama mikono na kwingine ni rahisi kuziona kwa kutumia lenzi ,lakini kama ni sehemu zilizojificha, huwa siyo rahisi kuzijua wala kuziona.c] Muwasho wa scabies hutokea kuwa mbaya zaidi mara baada ya kuoga,zaidi maji ya moto ,lakini wakati mwingine na ya baridi pia,.kama ilivyo kwa rafiki yako.[d] Hali ya muwasho wa wadudu hawa huongezeka zadi kipindi cha usiku.[,ambacho wote huwa tunalala,.na tunakuwa tumetoka kazini]MATIBABU;Ni baada ya kugundua uwepo wa burrows, Hivyo aende kwa daktari wa ngozi akaangaliwe vizuri.Na pia apimwe vizuri hicho kifua na Xray isomwe vizuri na Mwenye uelewa.,huo ni muda mrefu toka aanze kukohoa.
NEXT
***=CHINI YA MAKALIO,II; Katika kundi hili la pili PRURITUS inaweza kusababishwa sababu za ndani [a]magonjwa ya ini kushindwa kufanya kazi kwa figo [c]upungufu wa madini ya chuma [d]kisukari [e]thyroid [f]Cancer .Mfano kama Hodgkin's disease, ambapo muwasho hutokea mapema,zaidi kabla ya tatizo,na muwasho wake huenda bila mabadiliko yoyote kwa upande wa ngozi. NENDA HOSPITALI YA RUFAA,AANZIE KWA DAKTARI WA NGOZI KWANZA,KUWASHA HAKUWEZI KUPONA BILA KUTIBU UGONJWA ILIOUSABABISHA
.kuwashwa kwa jamaa yako bila mlipuko wa ngozi naweza kuuweka katika kundi la GENERALIZED PRURITUS [intense itching of the skin without eruption].PRURITUS huwa ni dalili [SYMPTOM] inayowakilisha ugonjwa, hivyo muwasho huo huhesabiwa kama moja ya dalili kiashirio cha ugonjwa Fulani.Muwasho kama wako kwa jinsi ulivyouelezea unaweza kudondokea katika makundi mawali[1] Unaosababishwa na mazingira ya nje [surface causes].maadamu mazingira ya allergy umeyakataa kimaelezo na kitiba,..hali ya SCABIES, [also known as sarcoptic acariasis ] tunaweza kuiizingatia zaidi kwenye suala la ugonjwa wako.[a]Alianza kukohowa tangu mwezi wa pili kikohozi chake ni severe,sababu kinaambatana na mikoromo pamoja na kupumua kwa shida,hiki kikohozi cha muda mrefu ni pelekeo la kushuka kinga mwilini,hii ni moja ya vigezo vya kushambuliwa na wadudu hawa.b]Wadudu hawa huanza kuonyesha dalili kuanzia wiki nne mpaka sita,baada ya kuingia kwenye ngozi.Dalili zake ni muwasho,na mabadiliko ya ngozi kwa baadhi ya sehemu kutengeneza mistari ulionyanyuka[burrows],na wakati mwingine mwisho wa huo muinuko huonekana kama kamuumuko kama ka chunusi [bump]. NEXT[/QUOTE
hapo kwenye text colour elezea vizuri...
mara nyingi miinuko hiyo[burrows] huonekana zaidi kwenye vidole au katikati yake.,juu ya viganja,katika maungio ya mikono [ elbow ] ,kwenye maumbile ya [male genitalia] kwenye kiuno sehemu ya mzunguko wa mkanda na chini ya ******.michirizi ya kwenye ngozi sababu ya kujikuna.kama hizo barrows zitakuwa sehemu za wazi kama mikono na kwingine ni rahisi kuziona kwa kutumia lenzi ,lakini kama ni sehemu zilizojificha, huwa siyo rahisi kuzijua wala kuziona.c] muwasho wa scabies hutokea kuwa mbaya zaidi mara baada ya kuoga,zaidi maji ya moto ,lakini wakati mwingine na ya baridi pia,.kama ilivyo kwa rafiki yako.[d] hali ya muwasho wa wadudu hawa huongezeka zadi kipindi cha usiku.[,ambacho wote huwa tunalala,.na tunakuwa tumetoka kazini]matibabu;ni baada ya kugundua uwepo wa burrows, hivyo aende kwa daktari wa ngozi akaangaliwe vizuri.na pia apimwe vizuri hicho kifua na xray isomwe vizuri na mwenye uelewa.,huo ni muda mrefu toka aanze kukohoa.
Next
Kama kuna mtu anajua wapi anaweza kupata matibabu ya uhakika naomba aelekeze, Ikiwezekana na Jina la Doctor