Maria Roza nitampa true story ya ndugu yangu iwe tu changamoto kwake ingawa kwa huyu ndugu yangu hawezi jenga tena ndoa yenye afya baada ya matatizo makubwa.
Huyu dada alikuwa anaishi kwa amani na upendo na mumewe yaan aseme nini asipewe maisha yalikuwa mazuri kwa kipindi kirefu sana bila kuhisi chochote kwa mumewe.ghafla mume akabadilika akaanza kuchelewa kurudi mara harudi mwisho akatoa kali kumwambia dada sio kwamba yeye sio mzuri au hamuhudumii vizuri ila kapata msichana anaempenda sanaaaa na akamuaga anaondoka pale home akachukua briefcase yake tu yenye docs muhimu akasepa.
Baada ya muda kidogo akabadili na dini akafunga ndoa kiislam huku dada kuchanganyikiwa basi akaingia kusali sanasana maisha yakaendelea tukawa tunapishana tu na shem na mke mpya barabarani magari yote walichukua basi watoto waliozoea magari wakaanza kupanda daladala huku home mke akapangisha nusu ya jumba lao ili ajikimu maana hata ada ilikuwa shida.miaka ilikatikayule jamaa akaanza kuumwa kwa sana mpaka akalala kitandani unajua alichofanya yule mke mpya? Akampigia sister eti njoo umuuguze mumeo mie niko bize sana na majukumu mengi.
Basi mdada mbio kwa sababu ya mapenzi na mumewe uguza na wewe pika michemsho akatafuta na doctor akapata dawa nzuri jamaa akasimama akapata afya.Guess wat????alivyopona kabisa akamwambia dada asije tena pale mke wake atakasirika na kumbuka demu alishasepa kitambo alienda panga nyumba ingine.Basi demu akarudi kwa nyodo nataka hati za nyumba na gari jipya akapewa vyote maisha yakaendelea mdada akawa anajirusha tu na mabwana wengine yule baba akaanza kuwa na mawazo na hivi hapati lishe nzuri na bado anaendelea kufanya lile tendo akadhoofu sana akaumwa mbaya demu akamkimbia tena eeti kapata kazi mkoani.akaondoka kamwacha kitandani dereva wake akamfata sista kumwambia jamaa anakufa kule. dada mbio na makapu ya huduma jamani, hudumia weee akaanza dozi upya mpaka akapona
Hapo akarudi home sasa ndoa tena haikuwa ndoa sista yuko fiti haumwi jamaa ndio hivyo tena. Basi sasa hivi wanalea tu familia na yeye kuhudumiwa sista kapendeza na wala hataki mchumba wala mume mwingine. yule mumewe anaishi mle ndani kwa chumba tofauti.lile demu liko huko mkoani,anaendelea kusambaza na ni msomi ile mbaya. Si kwamba hajarudiana nae sababu anaumwa, anasema mapenzi yaliisha tena akawa anamuhurumia tu.Unaona maisha yalivyo, wanaume wanajidanganya wanapendwa kumbe inapendwa pesa tu hapo wakitetereka mtu anaonyesha makucha yake.
Ushauri wangu huyo dada aendelee na maisha yake asiruhusu kitu kama hicho cause once huyo mume keshapenda mwingine na roho ikipenda hula nyama mbichi asilazimishe kusubiri mpaka yamkute huko aruddi wakati maisha yanaendelea. Bora aishi mwenyewe na mtoto wake awe happy. kuwa na mke mwenza ni kukaribisha maradhi ya moyo ambayo utakufa na mwanao atapata shida. dah sor kwa comment ndefu