Uchaguzi 2020 Msajili aonya mpango wa vyama kuungana Oktoba 3

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa nchini Sisty Nyahoza, ameviasa vyama vya siasa vinavyotaka kuungana siku ya Oktoba 3 mwaka huu, kuacha mara moja mpango huo kwani wanakiuka utaratibu wa sheria na kwamba walianza vizuri hivyo ni vyema kila mmoja akaendelea kunadi sera zake.

Nyahoza ametoa kauli hiyo hii leo Oktoba Mosi, 2020, kwenye kipindi cha Supa Breakfast ya East Africa Radio na kuongeza kuwa hata hivyo tayari Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imekwishaviandikia barua vyama hivyo kwa kuwa ni masuala ya kiofisi huwa hawaziweki barua hizo hadharani.

"Kwanza tunaawaasa hao wanaotaka kufanya hivyo tarehe 3 sisi kama walezi wa vyama vya siasa kwa sababu wanakiuka sheria, walianza vizuri hivyo kila mmoja aendelee kunadi sera yake na wagombea wao wa urais", alisema Nyahoza.

Amesema sheria ya vyama vya siasa inawekwa kwa maslahi ya wanachama na wananchi na unapotaka kushirikiana hutakiwi kufanya kitendo chochote kinachohadaa wananchi kwa hiyo ni kosa kufanya hivyo ghafla wakati wa uchaguzi.

“Ukiunganisha nguvu na chama kingine wakati mmeshakubaliana na wananchi kwamba mtatekeleza sera gani ni kuwahadaa, sisi tulishawasiliana nao na tukawaambia waache," alisema Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa nchini Nyahoza.

Vyama vya siasa vya upinzani vya ACT-Wazalendo na Chama Cha Demokrasia na Mandeleo (Chadema) vimekuwa vikitajwa kuwa na mpango wa kumuunga mkono mgombea mmoja wa urais Oktoba 3, licha ya kuwa vyama vyote hivyo vimeshasimamisha wagombea wao wa urais.
 
Nikipewa Urais wa siku moja,kufikia saa 10am mswaada wa kufutilia mbali ofisi hii utakuwa umeshawasilishwa bungeni,vyama vyote vya kisiasa visajiliwe Home affairs na kupeleka usajili wao tume ya uchaguzi.
 
Sisi wananchi wala hawatuchanganyi, sisi tunaelewa mbivu na mbichi. Kama ni kuchanganyikiwa ni wewe msajili. Wananchi tukopoa. Wakiungana tukiwapenda twawapa kura tusipowapenda twampa mwingine.
Halafu msajili kuwa muelewa, acha kufanyia kazi vyombo vya habari, acha kufanya siasa. Simamia sheria. Wewe unauhakika gani wanaungana?
Siku hizi viongozi kwenye ofisi za uma wanapwaya sana.
Kumbuka serikali inafanya kazi kwa Sheria, Kanuni na Taratibu. Zitumie
 
Ni kweli wamechanganyikiwa kwa sababu kila siku wanapata pressure kutoka kwa Jajambazi muovu kuwa "wakiungana wataning'oa miye " Inye mvua jua liwake Jambazi ni lazima achie ofisi takatifu! Kuna mtu aliyepelekwa kuzimu amerudi ana maagizo ya mwalimu Nyerere
 
Sasa kama chama hakina fedha za kuendelea kufanya kampeni waendelee tu ilihali serikali imewabana? Wakitaka wawape fedha watu wafanye kampeni, na waruhusu mabeberu waingize fedha zao
 
Why NEC wanapatwa na kiwewe?

Sasa kama wananchi wanahadaliwa, shida ya NEC ni nini? Acheni Wananchi waamue wenyewe. Mbona NEC walipiga kimya wakati yule mwingine alipokuwa anawahadaa wananchi kwa kutumia lugha isiyo ya Taifa live on National TV?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…