Msajili: Vyama vya kisiasa vitakavyohusika na fujo vitafutiliwa mbali

Msajili: Vyama vya kisiasa vitakavyohusika na fujo vitafutiliwa mbali

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Msajili wa Vyama vya Kisiasa Anne Nderitu ametisha kufutilia mbali usajili wa vyama vya kisiasa ambavyo shughuli zao zitakumbwa na ghasia kuelekea uchaguzi mkuu wa 2022.

Kwenye taarifa kwa vyombo vya habari Alhamisi, Bi Nderitu pia alivitaka vyamba vya kisiasa ambavyo wanachama wao walihusika katika ghasia zilizokumba chaguzi ndogo katika maeneobunge na wadi kadha wiki jana vijisafishe.

“Vyama vya kisiasa vilitia saini stakabadhi husika kwamba vitazingatia kanuni kuhusu mienendo mizuri kulingana na hitaji la Sheria ya Vyama vya Kisiasa. Kulingana na kanuni hiyo, ni sharti vyama vya kisiasa kudhibiti mienendo ya wanachama, maafisa, wagombeaji na wafuasi wao,” akasema Bi Nderitu.

“Kwa hivyo, afisi yangu haitasita kufutilia mbali usajili wa vyama vya kisiasa ambavyo vitakiuka hitaji hili la kisheria kwa kuruhusu shughuli zao kukumbwa na ghasia kuelekea uchaguzi mkuu ujao. Vyama ambavyo wanachake wao walisababisha ghasia katika chaguzi ndogo zilizopita pia sharti viwaadhibu kwa mujibu wa sheria,” akaongeza.

Bi Nderitu alisema kulingana na kipengele cha 91 cha Katiba, vyama vya kisiasa havipaswa kuhusishwa au kushiriki katika fujo, kwa kutoa vitisho au kushambulia wanachama wa vyama vingine pinzani vya kisiasa.

“Vyama vya kisiasa pia havipasi kushiriki ufisadi, kupokea au kutumia pesa haramu na kutumia rasilimali za umma isipokuwa fedha ambazo zimetengewa kupitia hazina ya vyama vya kisiasa,” akaeleza Msajili wa Vyama vya Kisiasa.

Bi Nderitu alilaani vikali fujo zilizoshuhudiwa katika wakati wa chaguzi ndogo katika maeneo bunge ya Matungu na Kabuchai na katika wadi za London (Nakuru) na Kiamakoma (Kisii).

Aliyekuwa Waziri wa Michezo Rashid Echesa Jumanne aliachiliwa huru kwa dhamana ya Sh1 milioni kwa kosa la kumchapa afisa wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) katika eneobunge la Kabuchai, Kaunti ya Bungoma.

Wabunge wengine 10 walihojiwa na maafisa wa Tume ya Kitaifa ya Uwiano na Utangamano (NCIC) siku hiyo hiyo kuhusiana na ghasia zilizoshuhudiwa katika chaguzi ndogo katika maeneo hayo matatu ya uwakilishi.

Nao wabunge Nelson Koech (Nelson), Wilson Kogo (Chesumei), Didmus Barasa (Kimilili) na Seneta wa Nandi Samson Cherargei walishtakiwa katika mahakama moja ya Bungoma kwa tuhuma za kuhusika katika fujo zilizokumba uchaguzi mdogo wa Kabuchai.
 
2022 uchaguzi? Au umeoteshwa kuwa tayari nini? Mi simo! [emoji849][emoji849]
 
Back
Top Bottom