Hapo nimekusoma. Naitamani Prius 3rd gen ila naogopa Battery ikifa.
Kinacho ua battery ya hybrid ni joto mkuu, na joto nikutokana na mmiliku kutofanya service ya kusafisha au kubadlidsha filter ya feni inayopoza hybrid battery ambayo inapatikana kwenye kiti cha nyuma cha abiria, ukiwa unafanya regular service ya kuipuliza na upepo ile filter kuondoa vumbi lililogandia pale basi hybrid battery inakaa muda mrefu sana infact Toyota Prius ni gari reliable kuliko hizi regular cars na ina low maintenance costs kuliko gari za kawaida... Mie nanayo 2 generation..very reliable, dependable and durable car ilikuja na km50,000 now ina 170,000+km with no single issue....
Cha maungi ukinunua prius gen ya 3 zingatia service ya
1. Fan ya kupoza hybrid battery
2. Kufatilia uzima wa water pump inaYozungusha maji ya kupoza inverter pamoja na gearbox
3. Water pump inayozungusha maji ya kupoza engine (kumbuka third gen inakuja na electric water pumps zinazozungusha maji ya kupoza engine lakini pia maji ya kupoza inverter na gearbox) so hii electric pump kuna wakati zinakufa na usipojua dalili za water pump kufa unaweza kuua engine au Inverter though hii ni extreme case kwakua gari ipo na protection mechanisms before hizi catastrophic issues kutokea
4. Kingine cha kuzingatia ni service ya kusafisha EGR system basi..
Kumbuka gen 2 Prius haina mambo mengi kama prius gen 3 na kuendelea because of absence ya baadhi ya mifumo mfano engine ya gen2 haina EGR system, ina electric water pump moja tu ya kuzungusha maji ya kupoza hybrid system, but upande wa cooling system ya engine inatumia mechanical water pump inayozungushwa na engine pale engine inapowaka.. pia prius gen 2 hazina filter kwenye fan inaYopoza battery but ikitokea unapenda endesha vioo wazi basi itajaa uchafu but kama vioo juu basi fan haitakuja kukupa tabu kwa kujaa uchafu..
Common issue kwa Prius gen 2 ni
- buti kuvujisha maji na kuleta changamoto kwenye hybrid system na battery japo issues zinakua solved kwa cleaning na kuziba kwa silcon mahala maji yanapenya..baada ya hapo unasahau shida.
-Kingine ambacho ni problem kwa prius ni kuharibika kwa water pump ya kupoza hybrid, but hii tatizo una replace hyo pump unasahau shida (mie niliweka ya pump ya BMW mpaka kwasho no issue..
-kingine kwa prius gen 2 inachangamoto ya dasnboard kuto onesha kitu occasionally...but this is very simple problem ambayo ukitaka permanent solution ni kufungua dasnboard, inatoa ile odometer una replace two capacitors ambazo hufa with time na kupoteza uwezo wake wa ku store charge, capacitor hizi zinauzwa buku buku but ukienda kwa fundi gari anaweza kukupiga hata 50k kuzibadili, but ukitaka ku solve hii issue temporary kila mara linapotokea basi unazima na kuwasha headlamp huku gari ikiwa off frequently mpaka kale ka alama ka kuonesha taa za parking zipo on kwenye dashboard kaonekane, kakisha onekana tu basi washa Gari dashboard itafanya kazi kama kawaida...