new generation
JF-Expert Member
- Mar 14, 2012
- 817
- 1,687
- Thread starter
-
- #21
gari za hybrid zinakuja na battery 2, battery moja ni ya kawaida ile ya 12V na hybrid battery yenye 201Volts, kuendesheka kwa kwa Gari ya hybrid endapo battery ile ya hybrid ikifa itategemea na set up ya hybrid system ya specific car manufacturer..mfano set up ya hybrid ya Honda ikitokea hybrid battery imekufa unachukua alternator na starter unaweka kwenye engine gari inaendelea kufanya kazi kama utaona hybrid battery kununua ni gharama, but kwa set up ya Toyota kidogo ipo tofauti. Hybrid ya Toyota ina tengenezwa na mota mbili zilizomo ndani ya gia box ambazo zipo connected ni engine pamoja through planetary and sun-gear set. Sasa engine ya Toyota hybrid inawashwa kwakutumia mota ya giabox ambayo hiyo mota ndo inafanya kazi kama starter na pia kama generator kujaji battery..but hii mota inazungushwa na umeme wa three-phase unatokana na hybrid battery, but battery ya gari haina three phase current ya kuzungusha mota ili engine iwake...so Gari haitawaka (ukumbuke gari ya hybrid haina starter wala alternator kama Gari ya kawaida, hiyo ile battery ya v12 haina kazi ya kuwasha gari, bali ni kutoa umeme kwenye system za Gari zinazohitaji umeme wa v12 kama vile radio, taa, fen, na ku run computers za Gari..Mkuu hivi in case battery imekufa unaweza endelea tumia gari kama kawaida kwa upande wa mafuta.
Pia kingine kinachofanya gari ya hybrid ya Toyota ifike muda isitembee kabisa endapo hybrid battery ikifa kabisa ni kwamba engine ya Toyota hybrid hiendeshi ile gari endapo mota zitakua hazina power ya kuendesha gari, engine pale ni generator, so mota inaitwa MG2 ndo mota inayoendesha ile gari ya Toyota na ndio mota inayoshirikiana na mota ya kuwashia gari kuweza ku badili gear ratio ili kupunguza rpm ya engine..(ukumbuke hybrid haina giabox kama gari ya kawaida yenye torque converter, sijui clutch, siju valve seal no gearbox ya hybrid it has less moving parts,..ni mota 2 na planetary gear Carrier hakuna kingine so ndo maana gearbox ya Toyota prius haifi kwakua haina kitu cha kuharibika, na Hydraulic fluid inayowekwa kwenye gear box kazi ni kupoza tu windings za mota na hukun kingine inafanya tofauti na gari ya kwaida). Therefore kutokana na sett up hii Toyota prius ikitokea battery imekufa kabisa au hybrid battery imeacha kufanya kazi kwa sababu yoyote ile japo haitokei basi gari haitawaka na kama itawaka basi haitaweza kutembea kwakua mota hazitakua na power ya kuzunguka na kuendesha gari...(but before kufika hapa gari yenye ipo na very advanced battery management mechanism ya kuku taarifu any fault ambayo ipo kwenye mfumo mzima wa hybrid kabla kufika hatua ya kuacha kufanya kazi (yaan kama regular cars zilivo)
Kingine battery sio lazima ununue nzima, ni unabadlli cell inayozingua unaweka nyingine gari inaendelea kutembea...mfano Toyota Prius ina battery pack 28 na kila pack moja ina vibattery vidogo 6 venye volts 1.2 kwa kila moja, hivo pack moja ina volts 7.2 ambazo zipo connected in series na kufanya box lote la hybrid battery kuwa na Dc voltage 201.6 but kwakua mota inahitaji three phase alternating current (AC) hapa ndo inverter inakuja kutumika kubadili DC 201.6 V to three phase AC voltage ya 650 kuendesha mota inayoendesha gari, ku power ac compressor. Na ku power stater ya engine. Ili ku-monitor voltage ya kila pack kuna sensor zinaweka kwenye kila module ya pack ili computer iweze ku detect tatizo na ku localize tatizo to specific pack ili iwe rahisi ku replace hiyo pack yenye shida..na mara nyingi issue inakuwa ni corrosion, so ukipiga msasa kwenye hiyo corrosion basi battery ina back to life, but kwa case pack ikifa basi unatoa pack unaweka nyingine maisha yanarudi na pack moja ina range kati ya Tza 70,000 to Tzs 120,000 so ni cheap sema watu wanatishwa na mafundi wasiojua hata hybrid inafanyaje kazi..but ni Gari nzuri sana na very easy to repair na ku maintain..(note sipeleki gari kwa mafundi natengeneza na kuservice mwenyewe Gari yangu kwakua mafundi wengi ni pasua na hawazijui Gari za hybrids