ClearingAgent
Member
- Nov 15, 2022
- 29
- 26
Utangulizi
Uzi huu unatoa maelezo kuhusu taratibu muhimu ambazo watumishi wa umma wanatakiwa kuzingatia wanapohitaji msamaha wa ushuru kwenye vyombo vya usafiri(magari/pikipiki).
Aina ya vyombo vya usafiri vinavyohusika na msamaha
(a) Magari
Ushuru unaosamehewa
Mtumihi wa umma alietimiza masharti yote yanayotakiwa kwa mujibu wa sheria atasamehewa kulipa ushuru wa forodha(ikport duty) tu. Kodi na ada zingine kama kodi ya ongezeko la thamani(VAT), ushuru wa bidhaa(Excise duty) na ada za usajili atatakiwa kulipa.
Taratibu muhimu za kufuata
NB: Kwa ambao wanaagiza vyombo vya usafiri toka nje wanatakiwa kufanya utaratibu wa kupata msamaha wa ushuru wiki mbili kabla ya chimbo husika hakijafika hapa nchini.

(b) Pikipiki za aina zoteMagari madogo aina ya saloon
Magari aina ya pick-up yenye uwezo wa kunena mzigo usiozidi tani mbili
Magari mengine yasiobeba zaidi ya abiria tisa
Gari yenye uwezo wa injini isiozidi 3000cc
Gari yenye umri chini ya miaka kumi tangu lilipotengenezwa bila kujali miezi
Ushuru unaosamehewa
Mtumihi wa umma alietimiza masharti yote yanayotakiwa kwa mujibu wa sheria atasamehewa kulipa ushuru wa forodha(ikport duty) tu. Kodi na ada zingine kama kodi ya ongezeko la thamani(VAT), ushuru wa bidhaa(Excise duty) na ada za usajili atatakiwa kulipa.
Taratibu muhimu za kufuata
Barua ya utambulisho kutoka kwa mwajiri.
Salary slip ya mwezi wa karibu.
Barua ya kuajiriwa kazini/Barua ya kupandishwa cheo.
Nakala ya kitambulisho cha kazi.
Picha 4(passport size) kwenye fomu ya maombi.
Namba ya utambulisho wa mlipakodi(TIN).
Kumbukumbu za ununuzi au uingizaji wa chombo husika cha usafiri hapa nchini.