Msamaha wa VAT

MAMA POROJO

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2007
Posts
4,974
Reaction score
785
Huu msamaha wa kodi ulilenga kwa mtu mmoja au kikundi cha watu, angalia code za product kama waziri alivyoziweka.

Product code alizoweka ni za kiwanda kinachotengeneza hizo product, kwa maana nyingine ni kuwa waziri alipelekewa quotation ya vifaa naye akavitangaza hivyo hivyo kama quotation aliyopelekewa asemehe VAT bila kupunguza wala kuongeza.

Tatizo litakuja wakati Mtanzania mwingine atakapopeleka quotation yake wizarani ikiwa na items sawasawa na alizotangaza waziri lakini zikiwa na code tofauti kutoka kwa mtengenezaji mwingine. Msamaha wa kodi hautatolewa.

Kama kuna mwenye uzoefu na mawazo tofauti atusaidie, kunusuru wafugaji wasije waikaingia mkenge kwa matarajio ya kupata msamaha wa VAT.
 
Hapo kuna shida , ina maana hizo Code lazima zitakuwa ni za Producer na si za TRA.Kama za TRA manake ni Categorization Codes for Exemptions, na kama za Producer basi lazima zitakuwa zimelengwa kwa Product za Producer mmoja tu, ukileta product ya mtu mwingine hawataitambua.
 
Product code alizoweka ni za kiwanda kinachotengeneza hizo product, kwa maana nyingine ni kuwa waziri alipelekewa quotation ya vifaa naye akavitangaza hivyo hivyo kama quotation aliyopelekewa asemehe VAT bila kupunguza wala kuongeza.

Hapana Mkuu, hizo ni codes za customs! Zipo very specific na waziri naamini ameziweka makusudi ili kuondoa usumbufu. Kwa mfano, akisema tu 'milk cans' haitoshi kuondoa utata hivyo kwa kuweka hizo codes amekuwa more specific ni vifaa vya aina gani kwa sababu hizo codes zote zimekuwa defined kwenye customs handbooks na zinatumika almost duniani kote

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…