Msamehe baba'ko, mbona Q-Chief aliweza?!

unavuna ulichopanda tu! kusamehe amesamehe lakini sio kuingilia kushirikishwa kwenye njia za mafanikio yake

lakini mzee alisema wanamahusiano mazuri na anamtuza.

alafu pia mbona anawatoto wengi tu kwa nini kila siku Diamond?
Si ndio mwenye nazo. Angekuwa bado anauza mitumba unadhani hata angekuwa na time nae. Ukitaka kujua idadi ya ndugu ulionao kuwa na vijisenti, hata yule mtoto wa rafiki wa kaka yake mjomba'ke bibi atasema ni binamu yako wa damu.
 
Hali halisi mtoto analelewa na mama muda wote hata kama watakuwa ndani ya ndoa lakini likitokea ndoa ikaleta mkwaruzano wakatengana bado mtoto ataenda na Mama yake na mda utakavyokuwa unaendelea Baba atakuwa akipeleka huduma kwa watoto lakini bado mzazi wa kike ataendelea kuwalisha sumu watoto kuwa kawaelea mwenyewe bila kusaidiwa na baba watoto na hiyo kuwajengea chuki na baba yao, na watoto wanapokuja kuwa watu wazima wanatakiwa kutumia busara kwa wazazi wao hao!
 
Nduli IDD amin Dada mond bin laden jinni gaidi
 
Uache kufatilia mambo ya watu
Huyo baba yake mwenyew alishakufat nakukwambia hawaelewani na mtoto wake au unaparamia maisha ya watu?mambo ya kwenye magazeti unayaamini?hujui wanatafuta hela hao kwa kuuza habari!acha kiherehere wewe
 
Shangaa huyu mtoa mada kwa kumjudge mwenzie!!
 
Itakua anajifanya ana huruma mbele y macho y watu lkn moyon ana kidonda
Ya nn sasa
hapo sasa ya nin sasa kuigiza maishadiamond ndio ana feel kinachomkuta so as long as hajaamua kuyasema why hamsaidii mzaz wake tumuachie mwenyewe na maisha yake...
 
Yaani hata Mimi mateso ya baba ndo furaha kwangu , baba alitutelekeza tena kwa kumuaibisha mama na sisi mbele za watu , akaoa mwanamke mwingine wakawa wanaishi mtaa wa pili kwa hiyo tunashuhudia maisha yao ya raha kwa macho yetu , mama etu alipitia tabu sana kazi alishaachishwa na akawa anapika pombe za kienyeji na baadhi ya wateja alikuwa analala nao tukishuhudia hii yote ili atutunze na mdogo wangu wa kike, .....in short maisha ya tabu tabu tabu ila namshukuru Mungu tulifanikiwa kusoma tena kwa kusomesha na shirika la watoto ya tima saivi wote tuna kazi na maisha yanaendelea....tulibadilisha majina ya ubini tukaandika ya babu mzaa mama.....huyo baba yupo Morogoro watoto wake wote wawili wavuta bangi hawa future kutokana na malezi ya kudekezwa na sasa Mzee kafilisika, mama etu alifariki kwa HIV naamini chanzo ni yeye baba kumtelekeza mama na watoto wake...... kamwe hatutamsahau huyu baba katili na huwa anatuma watu ohhh baba enu ana shida sijui anaumwa , huwa nawafukuza , yaani ukinitajia baba tu hata kama nikuqa kwenye raha zinayeyuka ghafla jinsi nisivyompenda tena niliwaambia wapambe wake siku akijitosa kunifuata kwangu ntachomfanya hataamini !......Kamweee abadaniiii siwezi kumsamehe....

Diamond shikilia Uzi huo huo ili iwe fundisho kwa mibaba mbegu, kupitia wewe Diamond mibaba mbegu mingi imejirekebisha na kwa sasa wanaume wanaokataa watoto idadi inazidi kupungua sana.
 
Mibaba kama hiyo hakuna kuisamehe inaumiza sana moyoni...tena wewe una huruma ingekuwa mimi ningesham RESTISHA IN PEACE.
 
kila kitu hutokea kwa sababu ,huenda babaake angemtunza asingekua hapo alipo. Hivyo amshukuru Mungu kwa yote na asamehe tu
 
Wanasema malipo ni hapahapa duniani Mbinguni ni adhabu tu
 
Ngumu ngumu tu,,maisha kama kwa mzungu,,,kwani anamtoto mmoja tu mpaka ang'ang'anie,,hata mi angekuwa baba yangu angechukua kavu tuu,,nayeye avumilie njaa tuu,,kila mtu na wakati wake.
 
kama mtu hujawahi kutelekezwa au kutohudumiwa na baba ako ilihali yu mzima wa afya na ni baba halali
utaona diamond ana roho mbaya sana..
ila kamaumewahi unaweza kuungana na diamond.
unaishi na mzazi mpaka anakua adui yako, hujui thamani yakuwa na baba...
umepitia mengi...
jamani acheni!!!!
huyo baba hana neno la kumpa diamond akasikia..
na haya yote diamond anayafanya kazi kwa bidii zote ni kutokana na hasira ya maisha aliyonayo!
huwezi kujua amepitia mangapi.
mpeni break!!!
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…