Msameheni bure Job Ndugai, amechanganyikiwa baada ya kuomba msamaha batilifu uliokataliwa! Barua yake ya Kujiuzulu nayo pia ni batilifu!

[https://res]

Baada ya kuibuka kwa mitazamo tofauti baada ya aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai kujiuzulu, tumemtafuta aliyekuwa Spika wa Bunge kuanzia 1994 hadi 2005 Pius Msekwa kwaajili ya ufafanuzi.

Msekwa ameeleza kuwa taratibu zote zimefuatwa na hakuna kilichoharibika kwa mujibu wa katiba ya Tanzania.

''Spika amechaguliwa na bunge, kwahiyo utaratibu sahihi barua ya Spika kujiuzulu ni lazima ipelekwe kwenye bunge na isomwe ndani ya bunge'' Spika Mstaafu Pius Msekwa ametoa ufafanuzi.

Zaidi msikilize hapa
 
Umeongea vyema mkuu, nchi inachezewa chezewa sana hii
Tuzidishe juhudi na kupaza sauti sisi sote kwa pamoja,adui yetu anaogopa UMOJA na ndiyo sababu anafanya figisu ili tusiwe na kauli moja.
Tudai Katiba itakayoshirikisha mahitaji ya Jamii pana ya wananchi wa Tanzania ya Tanganyika na Zanzibar.
 
CCM ndio Baba hapa kwetu, hivyo Ndugai inabidi aandike kwa Katibu Mkuu CCM tu, hana jinsi..

CCM ndio kila kitu, utake usitake, CCM yangu is a very powerful machine, ukileta maneno ya kijinga jinga, sijui nchi itapigwa mnada, CCM inakupiga mnada ww mwenyewe, ukome.. Ndugai kapigwa mnada si uona sasa!! πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

CCM safii kabisa.
 
Mkuu Learned Brother Petro mselewa, naunga mkono hoja kwa asilimia 100%, kilichofanyika ni kuhalalisha haramu na ubatili !.
P
 
Habari njema kwa watu wote, pendekezo No. 3 na No. 4 Katika bandiko hili, limetekelezwa kwa asilimia 100% kama lililopendekezwa.
Hivyo sasa ule ubatilifu katika barua ya Kujiuzulu kwa JYN umeondolewa kama nilivyo shauri, na kuwasilishwa barua halali,
Hivyo ile taarifa ya JYN kwa waandishi wa habari, kuwa ameandika barua kwa Katibu Mkuu CCM, sasa imebatilishwa na imefutwa kwenye website ya Bunge, barua rasmi ya kujiuzuli ni hii kwa Katibu wa Bunge, na CCM kupewa nakala.
Hongera sana Bunge letu tukufu kuubatilisha ubatili huu. Sasa kwenye hili la Spika umebaki ubatili mmoja wa Naibu Spika, Dr. Tulia Akson kujiuzulu u Naibu Spika, kabla ya kugombea Uspika.
P
 
Barua hii imezungumzwa tu mahakamani na wakili mkuu wa serikali, bunge halijazungumza kama limeipokea au la, na halijaeleza kuwa limepokea lini barua hiyo. Kimsingi ni kuwa haieleweki kama barua hii imepokelewa na bunge au la.
 
Kasome mapendekezo yangu hapa
kwenye uzi huu Je, wajua haramu isipoharimishwa inageuka halali? Na batili isipobatilishwa inageuka halali. Je, tuhalalishe ubatili huu kwa mhimili wetu wa Bunge? nilisema...

Habari njema kwa watu wote, pendekezo No. 3 na No. 4 Katika bandiko hili, limetekelezwa kwa asilimia 100% kama lililopendekezwa.
Hivyo sasa ule ubatilifu katika barua ya Kujiuzulu kwa JYN umeondolewa kama nilivyo shauri, na kuwasilishwa barua halali,
Hivyo ile taarifa ya JYN kwa waandishi wa habari, kuwa ameandika barua kwa Katibu Mkuu CCM, sasa imebatilishwa na imefutwa kwenye website ya Bunge, barua rasmi ni kwa Katibu wa Bunge, na CCM kupewa nakala.
Hongera sana Bunge letu tukufu kuubatilisha ubatili huu. Sasa kwenye hili la Spika umebaki ubatili mmoja wa Naibu Spika, Dr. Tulia Akson kujiuzulu u Naibu Spika, kabla ya kugombea Uspika.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…