Msameheni bure Job Ndugai, amechanganyikiwa baada ya kuomba msamaha batilifu uliokataliwa! Barua yake ya Kujiuzulu nayo pia ni batilifu!

Huyu mama ataendelea kuvunja katiba mpk tukome
 
Mkuu Pasko haya mambo yapo kiroho zaidi na sio kama wengi tunavofikilia .Haikuwa rahisi kiasi hicho Kwa Spika kukosea barua ya kujizulu sema ni kwa Sababu kiunabii Nchi yetu ipo GIZANI na hapa ni kama inasafishwa ili Giza liishe na hatimae tupate mwanga.
 
Ahsante sana mkuu P!
 
Tena hii barua inaonekana haikuchapwa na secretary kabisa maana hayo makosa ya CAP ON yasingekuwepo
 
Nakubaliana na wewe kabisa maana hata kama uwezo wake ni mdogo isingekuwa jambo rahisi Ndugai kushindwa kuelewa kwamba ataadhibiwa na chama chake kwa kwenda kuropoka hoja yake nje ya utaratibu wa chama chake. Ni upofu wa ki Mungu kwa maksudi mazuri yajayo kwa taifa letu.

Tuzidi kumwomba Mungu.
 
Katibu wa Bunge mwenyewe anajiona anawajibika kwa Katibu wa CCM. Angesema tu kuwa hawezi kufanyia kazi nakala lakini kama kawaida ya watendaji wetu, atafunika kombe tu. Haoni kuwa amedharauliwa!
Tabia hii ya kudharau Katiba na taratibu imetuharibia sana.

Amandla...
 
...Ndugai amepatwa na anguko baya kisiasa...ila anguko lake si zuri sana kwa uhuru wa mhimili aliokuwa anauongoza.

Ni vyema mtoa mada upitie upya athari za Uhuru wa muhimili wa bunge baada ya anguko la Ndugai baadala ya kuanzisha utitiri wa nyuzi kusherehekea anguko lake (nimeshauri tu).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…