Msameheni bure Job Ndugai, amechanganyikiwa baada ya kuomba msamaha batilifu uliokataliwa! Barua yake ya Kujiuzulu nayo pia ni batilifu!

Sawa Job Ndugai amechanganyikiwa waliopokea barua nao wamechanganyikiwa? kwa nini hawajaikataa? na kumwelekeza nini kinatakiwa kufanyika? Katibu wa ccm hajui katiba ya JMT inataka nini kwenye jambo hilo?
 

Mkuu,

Hiyo aliyoitoa Ndugai kwa umma ni taarifa na sio barua...ina kichwa cha habari kinachoeleza hivyo na hata mwanzo kabisa imeanza na maandishi haya "Naomba kutoa taarifa kwa umma...."

Ndani ya taarifa hiyo, ameeleza ya kwamba amepeleka barua ya kung'atuka kwake kwa wahusika aliowataja hapo...

Kwa mantiki hiyo, endapo ungeweza kuiona hiyo barua bila shaka ingekuwa na letterhead kama ambayo umeiambatanisha....
 
Wengi mnaiabudu ndo mana mpaka baadhi ya watu wanamfananisha raisi na Mungu, unapaswa kuheshimu ila kama yenyewe haijiheshimu kama ufanyaji wa kazi basi heshima lazima ishuke
Sasa simlikuwa mnasema speker ndugai untouchable, Mara akijaribu kaenda na maji, Sasa hiyo barua hata huyo zezeta wenu hajui imeandikwa saa ngapi na Nani,na Hana jeuri ya kuikana,

Jana Gwajima nae katuliza ball, kwisha habari yenu nyie Wahaini!
 
Mimi si mwanasheria lakini nilipoiona tu barua kwenye group la WhatsApp, nikawaambia wenzangu kuwa ni fake. Kitu cha kwanza kabisa, ni uandishi wa herufi kubwa barua nzima.

Tumefundishwa haya mambo shule ya msingi. Labda kama Ndugai aliruka primary. Nakumbuka kwenye mtihani wa mwisho wa Taifa wa kumaliza darasa la 7, kulikuwa na swali juu ya uandishi wa barua. Na ukiandika barua hivyo kwenye mtihani unapata sufuri. Ndugai ameongoza Bunge miaka yote hiyo kumbe hata kanuni za uandishi wa barua hajui! Ndio maana nchi yetu haipigi hatua. Herufi kubwa = unapiga kelele (shouting).

Pili, tumeona uvunjaji wa kanuni, taratibu na sheria katika utendaji wa Bunge chini ya Ndugai. Wabunge wasiokuwa na vyama kuendelea kuwa Wabunge chini ya Ndugai, kinyume na Katiba ya nchi. Kwa hiyo haishangazi kuwa hata barua ya kujiuzuru kwake haikufuata utaratibu uliowekwa na Katiba ya nchi.
Mhe. Job Ndugai, huku kutakuwa ni kutokana na kuchanganyikiwa tuu, barua hii nayo ni barua batilifu!,
 
Hahaahhah
 
Wewe mayala hiyo barua iliyoenda huko kwa katibu wa ccm na katibu wa bunge umeiyona kama haina letter head unayosema?? Mana hichi ulichotuma hapa ni taarifa kwa umma tu ambayo mwenye ndugai ameona aandike kuutarifu umma, barua iliyoenda kwa Katibu wa Bunge bado hatujaiona
 
Mkuu Pascal Mayalla ahsante kwa kudadavua vizuri.. mapungufu ni mengi sana.. Kuandika barua ya kujiuzulu kupitia memo.., kuipeleka kwa sehemu zisizo sahihi, kuandika kwa herufi kubwa kama 'Taarifa ya Polisi, - police statement, kutokufuata taratibu sahihi za kujiuzulu n.k.
Kwa watu wanaoangalia 'between the lines' utaona ama alimwandikia Katibu Mkuu wa Chama kwa kuwa yeye ndiyo aliyekuwa wa mwisho kumshawishi au barua iliandaliwa na watu wengine wasioelewa taratibu vizuri halafu akapelekewa..
Lakini mwisho wa yote lazima tukubaliana kuwa Katiba yetu haina kitu kinachoitwa Mihimili huru ila kuna mhimili mmoja ambao umejichimbia kuliko mingine..
Kumbuka Katiba yetu inasema Rais ni sehemu ya Bunge lakini si Mbunge..
 
Mungu wa Mbinguni asaidie Taifa la Tanzania. Kingunge wa watunga sheria asijue Sheria Kuu aka Katiba inaagiza nini anapo amua kujiuzulu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…