Msameheni bure Job Ndugai, amechanganyikiwa baada ya kuomba msamaha batilifu uliokataliwa! Barua yake ya Kujiuzulu nayo pia ni batilifu!

Ndugu Paskali, hiyo siyo barua ya kujiuzuru.... Hiyo ni taarifa ya umma, juu ya barua ya kujiuzuru ambayo amepeleka kwa katibu mkuu na kopi bungeni.

Nakubaliana na wewe amekosea kama kweli atakuwa ameaandika barua kwenda kwa katibu mkuu wa CCM na kuwapa Bunge kopi.. Hiyo barua haitaonyeshwa humu... Inawezekana hakuna barua yoyote..

Hapa tunaweza kuhoji tu utaratibu aliotumiwa kama ni sahihi au laa.. ambao ni batili.
 
Kwani amestaafu....[emoji16]...au tafsida imefanya kazi?
 
Wee pasikali unafikiri ndugai havijui hivyo vifungu?!!!!!
Kwa taarifa yako anavijua sanaaaa..
 
Asingejiuzulu ndio hata ubunge angenyang'anywa kwa kuvuliwa uanachama jumla.
Matola, unadhan yeye kubakia Mbunge, kutamwaminisha mama kua kaachana na mambo ya 2025 kama Mama alivyodai?

Ikiwa jibu ni hapana, Basi hata Huo Ubunge bado wanaweza mnyang'anya.
 
Kwani mhe Ndungai mwenyewe anasemaje ??!!!
 
Ex-supika sio wa kumhurumia batli si batili Analipa kwa yote aliyoyatenda
Mungu amemtumia kupigania haki ya wananchi (kuhoji mikopo mikopo) BUT Mungu ameutumia ujumbe wake kulipa gharama za matendo yake maovu....

Tunachoshindwa kutambua ni Dictatorship imeota mizizi
Kama mtawala anaona kuikosoa serikali ni dhambi tena kukosolewa na mwandani wao na akamuadhibu kiasi hiki iko shida kubwa...

Sisiem tambueni Mungu yupo mtalipa gharama kwa matendo yenu
Endeleeni kuumizana kuna siku mtawapigia magoti upinzani. Hili zoezi linaendelea mnayemsifia saaaaana atawamaliza kwa maneno ya kwenye kanga

Lindeni haki ya Taifa na wananchi
Epukeni kulibagua Taifa KIDINI KABILA NA KI-Uzanzibari na KI-Bara (hii dhambi inaota mizizi kwa kasi sana)

UBAGUZI UMETAMALAKI

Watawala wanaligawa Taifa kwa mitindo mitindo
 
Mambo ya ubatili nchi hii ni Mengi,sio hili tu,
Wale wabunge 19,WapO Bungeni kibatili
 
Alizingua kuomba radhi, hapo ndipo alipochemka, bora angejiudhuru na msimamo wake ningemuona shujaa...kazingua sana.
 
Tusifike huko, ubaguzi ni mbaya haufai na watanzania sio asili yetu kubaguana !! Mungu ibariki Tanzania !
 
Nachelea kusema alitumia njia batili kutoa tamko batili, Katika ile speech ya Job Ndugai katika kile kikao cha Saccos ya Wagogo alijitanabaisha kwa Ugogo zaidi kuliko UTanzania, kuna mahali akiwaeleza wagogo wenzie namna Alivyo tafiti kupia CDA kwa misingi ya Ukabila(kwasababu alimtaja mgogo mwenzie aliyempa nyaraka kuchunguza wakazi wa pembezoni mwa barabara) kisha akastaajabu pasina kukumbuka hii ni Tanganyika ambayo Mwl aliiasisi kwa kutaka matangamano ya makabila mbalimbali, Leo ukienda Oysterbay au hata pale Upanga kwa lengo lakutafuta nyumba za wazaramo utabuma, kiufupi ndugai ilikuwa lazima aachie nafasi ile mbali na kuwepo hiyo hoja ya Mihimili Mitatu Huru

Lakini pia ndugai ile speech yake kwanini ilitaja Habari za 2025 nae ni mwanaccm na kile ni kikao cha Wagogo alikuwa anaaddress audience ipi? Ya wana CCM wa Kigogo, Watanganyika wa Kigogo au wa Tanzania wote kwa ujumla? Na kwanini statement yake iliashiria kwamba kuna hofu nafsini mwake kwamba huenda akaenguliwa nafasi ya uspika au ngazi za juu?
Pascal Mayalla wewe ni bobezi kwenye nyanja Tofauti hivi hujatazama kwa jicho jingine speech yake? Au nawe umetazama kiclip tu

Nakupa homework lakini hili Tatizo ni kubwa si kwa udogo huo wa batili au batilifu, hilo Bunge la kuisimamia serikali bado halipatikana Achana na spika ambaye yeye ni mtu mmoja tu
 
Kwamba spika Ndugai kaamka vizuri Leo baada ya miaka yake yote katika kiti? Au ni msaka Tonge? Hizi fallacies of ethos zinapofusha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…