Msamiati mpya wa SUKUMA GANG haufai, unaweza kuleta matatizo kwenye jamii hapo baadaye. Mamlaka ziliangalie hili

Akawasaidia nn? Mbona mikoa yenu ni maskin sana kitakwimu?
 

..Magufuli ndiye aliyeuchochea ukabila ktk siasa zetu.

..kiongozi wa nchi anazungumza kwa kutumia lugha ya kabila lake mlitegemea wale wasio wa kabila lake watamuelewa vipi?

..na alipokuwa akipiga kampeni kwa Kisukuma wewe ulikuwa mmoja wa wachangiaji wa hapa JF mliomtetea bila kuchoka.

..Ni matumaini yangu kwamba Watz tutajifunza kutokana na makosa ya Magufuli, na tutaazimia kuyarekebisha.
 
Kuongea kisukuma mbele ya wasukuma haikuwa dhambi pengine kati ya hao aliyoongea nao kisukuma wapo hawajui kiswahili.

Hakuna mbunge mchagga aliyekatazwa kuongea kichagga mbele ya hadhira ya wachagga.

Hayupo mwanasiasa ambaye akiwa na wa kwao hachomekei maneno machache ya lugha ya kwao.
 
..mchagga angekampeni kilugha ingekuwa tatizo kubwa kwake na chama chake.

..vilevile tume ya uchaguzi imekataza wagombea kuzungumza kikabila.

..maelekezo ya sheria / tume ni kwamba wagombea wazungumze Kiswahili na kama kuna wasioelewa watafsiriwe hotuba na mkalimani.

..Ni bahati mbaya sana kwamba Magufuli alivunja sheria ya uchaguzi waziwazi na hakukuwa na mtu au mamlaka yoyote ya kumkemea.

..Magufuli ndiye aliyeuchochea ukabila hapa nchini. Na vita yake dhidi ya Chadema na kampeni kwamba ni chama cha wachagga matokeo yake tunayaona sasa hivi.
 
Hii karata ya ukabila ukiachia mbali Rais aliepita hutumiwa hata na ccm yenyewe. CUF waliisingizia ya wazanzibar na ni waislam wanaotaka kuvuruga amani ya nchi. Cuf ikayumba. Sasa hivi CDM wanasema ni chama cha wachagga ila this time hawakufaulu kukiuwa chama hicho kipo kinachechemea. Ccm imekuwa ikichezea amani ya nchi kama kitenesi. Generation ijayo watakuwa na mtazamo mwingine na hawatachotwa na hizi propaganda hatarishi na mapinduzi ya kiutawala na kisera yatakuja ba hakuna atakae zuia.
 
..kabla ya kuitwa chama cha wachagga cdm iliitwa chama cha wakatoliki, enzi zile km ni dr.slaa.

..halafu kulikuwa na chama cha udp kilichoanzishwa na john cheyo. Chama hicho kilisingiziwa kuwa ni cha wasukuma kwasababu cheyo ni mwenyeji wa bariadi shinyanga.
 
Nakubaliana na wewe. Unajua ukikosa hoja unaishia kuingia kwenye mbinu chafu. Naona sasa mbinu imebadilika ni vita juu ya wasukuma na wachagga. No hizi ni siasa sio makabila tumepoteza direction completely.
 
Naunga mkono hoja, na leo ndio the Gang has officialy been disbanded kwenye huu uteuzi mpya.
P
 
Bado aisee usitudanganye msomi, kunanakina Dotto hawajatoka wote waziri na KM, halafu kuna Mwigulu and the likes. So bado wapo
Japo the Sukuma gang ni just fictions, sio kila Msukuma aliyekuwa top was a member na pia japo jina ni Sukuma Gang, sio kila aliyepo ni Msukuma !.

The porpoted Sukuma Gang ni kile kikundi kidogo cha watu waliofanya siri kuugua kwa naniliu, na hata alipo nanilii, hawakutoa taarifa on time kwa the next in command kuwa naniliu amaisha nanilii!, wakatafuta jinsi ya kuzuia nanihii asiwe yeye!. Wasukuma wengine walikataa na aliyewadhibiti hao the Sukuma Gang, pia ni Msukuma!.

Mwanzo Wasukuma wengine wote ambao hawakuhusika kwenye mipango hiyo miovu, hawakuguswa, hawahusiki. Ile hoja ya kuchota mihela kwenye kibubu chetu ilikuwa ni uongo tuu na uzushi wa yule mzushi wa Twitter.
But now as times go by, naona kama sasa Wasukuma wanashughulikiwa!. Hili ni jambo la hatari sana!. Wasukuma ndio walio wengi, na ndio the determinant ya nani anakuwa rais wa nchi hii!.

Huku kuwabagua na kuwaengua Wasukuma, kukiendelea hivi hivi hadi 2025, Wasukuma uvumilivu ukiwaisha wakaamua liwalo na liwe, wanaweza kuamua...
P
 
Jitu Zuma ovyooo...
 
Well nakubaliana nawe lakini kumbuka nami namaanisha hao wachache niliowataja wapo kwenye hiyo gang especially huyo KM aliplay directly wakati wa maficho ya kifo Cha nanihii ili waweze kunanihii zile nanihii kule BOT na wakaendelea kumpanga nanihii ndio awe nanihii walihakikisha nanihii hapewi nafasi kwa kutumia hoja dhaifu za kikatiba ambazo zilikataliwa na msukuma mwenzao ambae alistukia huo mchezo wao na akawatosa.

So bado wapo although wanazidi kupungua nguvu maana jina linabeba wengi waliokuwemo humo pamoja nakubaliana nawe kwamba wapo ambao hawapo kwenye hiyo origin ya hilo jina kama bwana yule aliyepandishwa kutoka kuwa mwalimu wa chuo mpaka kufikia kuwa mtumishi namba moja🤷
 
huyo KM aliplay directly wakati wa maficho ya kifo Cha nanihii ili waweze kunanihii zile nanihii kule BOT
Huu ulikuwa ni uzushi tuu wa yule mzushi wa Twitter, ndio maana nanii baada ya kuingia tuu aliorder ifanyike special audit na ikukutikana hakuna uchotaji wowote, ila ni kweli fedha zilitolewa na ni kweli walihangaika naye kujaribu kumnusuru mara huku mara kule ila ndio hivyo tena, hivyo yule kijana ni safi.
P
 
Hahaha, umeandika yote Ila hiyo sentence ya mwisho umeharibu mzee. Huyo kijana Hana usafi wowote aisee kwanza sababu alikuwa member wa level ya juu sana kwenye Ile gang pia baada ya michezo yake mingi aliyopiga pasi za moja kwa moja na uncle wake.

Anyway nasikia wameamua kuform chama kabisa maana mzushi wa Twitter niliona ametonya sehemu na kutoa hadi Watsap charts zao. Kama ni kweli basi hawajamalizwa maana itakuwa inawezekana Ile nanihii iliyochotwa BOT basi ni kweli maana ilisemekana itatumika kutunisha mfuko wa gang ili iwe na power ya kwenye kura wakati wa uchaguzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…