Msanifu majengo aliyekataa kulipwa kwa kupanua misikiti miwili mitakatifu

Msanifu majengo aliyekataa kulipwa kwa kupanua misikiti miwili mitakatifu

Malaria 2

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2023
Posts
6,846
Reaction score
10,288
Mohamed Kamal Ismail alikuwa mmoja wa watu muhimu nyuma ya upanuzi mkubwa wa misikiti miwili mitakatifu nchini Saudi Arabia.
Msanifu majengo wa Misri, aliyezaliwa mwaka 1908, alichaguliwa na Mfalme Fahd wa Saudi Arabia kusimamia upanuzi wa Masjid al- Haram (Msikiti Mkuu wa Makka) na Masjid an- Nabawi (Misikiti ya Mtume) iliyopo Madina.
Upanuzi wa Masjid al- Haram ulielezewa wakati huo kama upanuzi mkubwa zaidi katika karne 14.
Licha ya juhudi za Mfalme Fahd na kampuni ya Bin Laden, Bwana Ismail alikataa kulipwa kwa kazi yake.
Alisema: "Kwa nini nichukue pesa kwa ajili ya kazi yangu katika sehemu takatifu zaidi duniani. Nitawezaje kukutana na Mwenyezi Mungu Siku ya Kiama?

Elimu na ndoa​

Bwana Ismail alikuwa mwanafunzi mdogo zaidi kuwahi kuhitimu shule ya sekondari (upili) nchini Misri na mtu mdogo zaidi kusajiliwa katika shule ya uhandisi ya Royal School of Engineering.
Kisha alipelekwa Ulaya kupata ujuzi zaidi katika usanifu wa Kiislamu.
Alioa akiwa na umri wa miaka 44, na mkewe alijifungua mtoto wa kiume kabla ya kufariki.
Bwana Ismail kisha akajitolea kumwabudu Mungu hadi kifo chake akiwa na umri wa miaka 100, na katika maisha yake yote alipendelea kukaa mbali na vyombo vya habari.

Marumaru nyeupe​

Bwana Ismail alikuwa msimamizi mkuu wa ujenzi wa kutumia marumaru kwenye sakafu ya Masjid al-Haram ili kukabiliana na hali ya hewa ya joto nchini Saudi Arabia.
Marumaru nyeupe nadra, iliyoingizwa kutoka Ugiriki, inajulikana kwa ubora wake usio wa kawaida, rangi nyeupe na uwezo wa kupoza nyumba zenye joto.
Mfalme Fahd baadaye alimuomba Bwana Ismail kutumia marumaru hizo hizo nyeupe katika Masjid an-Nabawi.
Masjid al-Haram, au Msikiti Mkuu wa Makka, ni mahali patakatifu zaidi katika Uislamu.
Umepitia hatua kadhaa za upanuzi wakati wa historia yake ili kukidhi idadi kubwa ya mahujaji

wanaotekeleza majukumu ya Hijja na Umrah.
Baada ya upanuzi huo wakati wa enzi za Mfalme Fad, msikiti huo ulikuwa na ukubwa wa mita za mraba 356,800 na unaweza kuwapokea waumini 820,000 katika siku za kawaida na zaidi ya milioni moja wakati wa msimu wa Hijja na mwezi mtukufu wa Ramadhani.
 
Huyo aliyepanua misikikiti na aliyejenga nyumba Mia moja za homeless ili wasife kwa baridi ni yupi kafanya zaidi?..
Kumbuka katika waumini 2B si yeye tu angewiwa kufanya hivyo,kuna wengi zaidi wanaweza kwenda mbele kidogo ama zaidi ya hapo.
Ila katika watu 8B kaonekana mmoja tu,uenda hasijitokeze mwingine.
 
Sasa Unapinga, unakosoa, unachukia au nini?
 
Huyo aliyepanua misikikiti na aliyejenga nyumba Mia moja za homeless ili wasife kwa baridi ni yupi kafanya zaidi?..
Kumbuka katika waumini 2B si yeye tu angewiwa kufanya hivyo,kuna wengi zaidi wanaweza kwenda mbele kidogo ama zaidi ya hapo.
Ila katika watu 8B kaonekana mmoja tu,uenda hasijitokeze mwingine.
alejenga nyumba 100?
 
Bin laden hapo kaharibu zoezi zima.

Unajenga nyumba ya ibada.

Baadae unatoka kwenda kutuma watu wakajilipue kuua wasiokua na hatia.
 
Back
Top Bottom