TANZIA Msanii Albino Fulani afariki dunia nchini Marekani

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
6,067
Reaction score
10,938
Msanii wa Muziki na Mwanaharakati wa haki za Watu wenye Ulemavu wa Ngozi nchini, Babu Sikare maarufu kama Albino Fulani amefariki dunia. Habari hizo za msiba zimetolewa katika ukurasa wa Twitter wa MwanaFa.

Pia soma > Mkasi - SO2E09 With Babu Sikare (Albino Fulani)

--
Jina lake ni Babu Sikare aliyekuwa na makazi yake makuu Columbus, Ohio nchini Marekani alikuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya. Jina lake la kisanii ni Albino Fulani , Amefariki Dunia nchini Marekani

albino.jpg

Albino Fulani enzi za uhai wake

Moja ya sanaa yake kati ya nyingi

=====

Babu Sikare maarufu kama Albino Fulani ambaye amewahi kutamba na nyimbo kadhaa ikiwemo "Nafasi" aliyoshirikiana na Mwana FA, Sugu na Belle 9 amefariki Dunia akiwa Nchini Marekani.

JamiiForums.com imezungumza na Mwana FA ambaye ni rafiki yake wa karibu amesema chanzo za Kifo cha Albino Fulani ni maradhi ya Saratani ya Ngozi ambayo aliwahi kupona siku za nyuma lakini ikarejea tena na kumsumbua hadi mauti yalipomkuta.

Mwana FA amesema alizungumza na Albino Fulani wiki kadhaa zilizopita ambapo alimpa taarifa kuwa Madaktari wamemwambia ana muda mfupi wa kuishi kutokana na Saratani yake kusambaa sehemu kubwa ya mwili wake na kuathiri Afya yake kiujumla.
 
Msanii wa Muziki na Mwanaharakati wa haki za Albino nchini, Babu Sikare maarufu kama Albino Fulani amefariki dunia. Habari hizo za msiba zimetolewa kati ukurasa wa Twitter wa MwanaFa.

Pia soma > Mkasi - SO2E09 With Babu Sikare (Albino Fulani)

--
Jina lake ni Babu Sikare aliyekuwa na makazi yake makuu Columbus, Ohio nchini Marekani alikuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya. Jina lake la kisanii ni Albino Fulani , Amefariki Dunia nchini Marekani

View attachment 2510396
Albino Fulani enzi za uhai wake

Moja ya sanaa yake kati ya nyingi

=====

Babu Sikare maarufu kama Albino Fulani ambaye amewahi kutamba na nyimbo kadhaa ikiwemo "Nafasi" aliyoshirikiana na Mwana FA, Sugu na Belle 9 amefariki Dunia akiwa Nchini Marekani.

JamiiForums.com imezungumza na Mwana FA ambaye ni rafiki yake wa karibu amesema chanzo za Kifo cha Albino Fulani ni maradhi ya Saratani ya Ngozi ambayo aliwahi kupona siku za nyuma lakini ikarejea tena na kumsumbua hadi mauti yalipomkuta.

Mwana FA amesema alizungumza na Albino Fulani wiki kadhaa zilizopita ambapo alimpa taarifa kuwa Madaktari wamemwambia ana muda mfupi wa kuishi kutokana na Saratani yake kusambaa sehemu kubwa ya mwili wake na kuathiri Afya yake kiujumla.

Bado alikuwa katika umri wa kupigana na maisha. Mungu amlaze mahali pema
 
Back
Top Bottom