Msanii Dully Sykes afunguka ya moyoni kuhusu mafanikio ya kupata pesa kwa Diamond Platnumz

Msanii Dully Sykes afunguka ya moyoni kuhusu mafanikio ya kupata pesa kwa Diamond Platnumz

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Posts
13,053
Reaction score
6,304
diamond%20amekaa_full.jpg

[h=1]Jina la Diamond Platinumz mtoto wa Tandale mwenye historia ya kuishi maisha ya ukata, sasa hivi ni moja kati ya majina makubwa kimuziki barani Afrika huku akishiriki kwenye project kubwa kama One Campaign iliyoongozwa na D’Banj huku akipewa mashavu na wasanii wakubwa wa Afrika Magharibi.[/h] Dully Sykes ameuambia mtandao wa Times Fm moja kati ya sababu ambazo zinambeba mwimbaji huyo na kumpeleka kwenye level ya juu ya mafanikio kuwa ni kiu kubwa aliyonayo inayomfanya afanye kazi usiku na mchana huku akiwasumbua maproducer bila kusubiri wamuite studio.
“Wasimuone Diamond anafanya vizuri, Diamond anafika mbali wakafikiria Diamond anafanya kazi kwa kumsubiria hadi producer amuite studio, no sio kweli. Diamond anashinda usiku kila siku studio.” Amesema Dully Sykes.
Dully ameeleza kuwa hata yeye pia hukesha studio akifanya kazi na ndio sababu inayomfanya aendelee kufanya vizuri tangu alipoanza muziki bila kupotea na kwamba wasanii wengi wasiofanya hivyo huishia kuporomoka na kudai kuwa walioko juu wanafanya uchawi.
Mwimbaji huyo ambaye ni mmiliki wa studio ya 4.12 ameongeza kuwa akili ya kuwekeza kwenye vitega uchumi pindi uwapo juu ni moja kati ya sababu zinazomsaidia msanii kuendelea kuwa juu kwa muda mrefu.
“Kama wangekuwa wajanja sasa hivi wangekuwa na vitega uchumi…kitu kama studio ni kama jiko. Unakula kwa kutumia studio. Hata kama mtu haji lakini unaweza kutengeneza muziki kwa kutumia akili yako ukasema ‘leo bwana nimeamka saa kumi ya usiku nina idea yangu hebu ngoja niingie studio nidumbukize hii sauti pengine kesho itanifaa. Na kweli unakaa unapata idea nzuri na unatengeneza kitu kizuri.”
Chanzo TIMES FM
 
vitega uchumi gani alivyokuwa navyo Dully zaidi ya hiyo studio, dhahabu record haikuwa yake kumbe?
 
" Dully ameeleza kuwa hata yeye pia hukesha studio akifanya kazi na ndio sababu inayomfanya aendelee kufanya vizuri tangu alipoanza muziki bila kupotea na kwamba wasanii wengi wasiofanya hivyo huishia kuporomoka na kudai kuwa walioko juu wanafanya uchawi.
Mwimbaji huyo ambaye ni mmiliki wa studio ya 4.12 ameongeza kuwa akili ya kuwekeza kwenye vitega uchumi pindi uwapo juu ni moja kati ya sababu zinazomsaidia msanii kuendelea kuwa juu kwa muda mrefu.

:target::help:
 
Ila kaongea kweli ukiangalia Jide ana Machozi band na Nyumbani lounge usipomsikia kwenye singo utamfata kwenye band ukimkosa kwenye band utamkuta mgahawani ilo linachangia jina lake libaki kuwa juu japo wapo akina Maunda wamekuja na kuondoka ila yeye bado yupo coz ajaconcentrate kwenye kuimba tu.
 
Swadata utakuwa umemuelewa vizuri dully ndio maana usipomsikia ata didy kwenye music utamsikia kwenye perfume, nguo etc
 
Swadata utakuwa umemuelewa vizuri dully ndio maana usipomsikia ata didy kwenye music utamsikia kwenye perfume, nguo etc

Yup ndo hicho wasanii walitakiwa kujifunza hawajui majina yao ni pesa tosha ukijua kuitumia mf. Rihana ana perfume zake kila mtu atataka kuzinunua sababu ya brandname hata mshindi wa BBA mwaka jana Dillish kaanzisha niashara ya lipstick kwa kutumia brand yake...
 
Ata beyonce ana perfume zake pia
 
vitega uchumi gani alivyokuwa navyo Dully zaidi ya hiyo studio, dhahabu record haikuwa yake kumbe?

Mjomba hata akiwa ana kitega uchumi kimoja ndo uwezo wake,
 
Kwa hiyo domo hua halali usiku anashinda studio na Wema je inakuwaje wanashinda naee auu
 
Kwa hiyo domo hua halali usiku anashinda studio na Wema je inakuwaje wanashinda naee auu

Msifuate magazeti sana,wema anatenga jamaa anaweka tudakika tuchache mara kadhaa,jamaa anaendelea kupiga kazi. Kazi na dawa.
 
Back
Top Bottom